MWANZA.
Bodi ya pamba imewaonya baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika (AMCOS) ambao sio waaminifu wanaokwamisha zoezi la usambazaji wa viuadudu vinavyotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa TCB mkoa wa Mwanza James Shimbe alikpokuwa akipokea viuwadudu kutoka kampuni ya Bens Agrostar na kueleza kuwa kuna baadhi ya watumishi wamekuwa wakipelekewa viuadudu na wao kutumia kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
" Ninawaomba sana wale ambao wanafanya hivyo kuacha tabia hiyo maana sisi hatupendezwi nao viuadudu ni kwa ajili ya wakulima na sio wao"Alisema James.
James ameeleza kuwa watu wa namna hiyo wanarudisha maendeleo nyuma hawataki kupoteza muda kwa sababu wanafanya kwa maslahi ya nchi pamoja na wakulima wa zao la pamba.
"Sasa wananchi wengi wanafanya kwa maslahi yao kwa sababu gani na sisi hatutaki hilo kujirudia" Alisema James.
Ameeleza kuwa serikali imezamilia kuzalisha zao la pamba kwa wingi ambalo ni zao la kimkakati hivyo halmashauri kuhakikisha wanafanya usimamizi.
Aidha amewataka wakulimakuondoa hofu kwani wako tayari kukabiliana na wadudu hao wasumbufu.
Ameeleza kuwa wataendelea kutoa elimu ya kutosha kuhusiana na wadudu wasumbufu katika mashamba, kuendelea kuwaelewesha matumizi sahihi ya viuawadudu na vinyunyuzi ambavyo wanawapelea endapo watatumia vizuri hawatakaa waone tatizo lolote lile.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Bens Agrostar Benson Mwalunenge ameeleza kuwa changamoto kubwa ya matumizi ya viuwatirifu kwa wakulima.
Benson ameeleza kuwa wanapokwenda madukani wananunua na kupewa maelekezo wanapokwenda kutumia wanashindwa kufata maelekezo na mwisho wa siku wanatoa malalamiko kuwa viwatirifu sio vizuri.
Hata hivyo amewasihi wakulima kabla ya kutumia kiwatilifu ambacho amenunua dukani ni vyema wakajua matumizi yake.
" kufanya jambo kinyume na maelekezo ndio kunapelekea kuharibu mazao, ila wakifata maelekezo watafanikisha dhima yao" Alisema Benson.
0 Comments