Header Ads Widget

WANANCHI ARUMERU WATAKIWA KUTEKETEZA MASHAMBA YA BANGI

 



 Na,Jusline Marco;Arusha


Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl. James Nchembe ametoa rai kwa wananchi waliopewa siku 14 za kuteketeza bangi kwa hiyari kutekeleza agizo hilo kabla ya hatua za utaifishaji wa mashamba hayo hazijachukuliwa kwa watakao kaidi agizo hilo.


 Mwl.Nchembe ametoa agizo hilo katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Arusha ambapo amewataka madiwani hao kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuhakikisha wanatokomeza kilimo cha bangi katika kata ambazo zinalima zao hilo.


Aidha amesema baadhi ya waheshimiwa madiwami ni wadau watokanayo na maeneo yanayofanya uzalishaji wa bangi hivyo kupitia oparesheni ya uteketezaji wa zao hilo hakutakuwa na uwajibishaji wa mtu yeyote bali mashamba ambayo yatakuwa na zao hilo yatataifishwa na kuwa mali ya serikali.



"Nawaagiza mkawaambie wenyeviti wenu wa vijiji na vitongoji kuwa serikali haijaenda likizo hivyo tunapopanga mambo yetu ya kadha wa kadha lazima tuangalie usalama wetu ukoje."alisema Mtembe


Ameongeza kama hatutafumbia macho suala hilo tutazalisha watanzania wala bangi ambapo madhara yake ni makubwa hivyo amesema oparesheni hiyo italenga kipiga vita ilimaji wa bangi na kutokomeza matumizi yake.


"Ninadhani wananchi wetu wakipigwa na njaa miaka miwili mfululizo na maeneo yao tukiyazuiya pengine akili zitawakaa sawa na nyie wsheshimiwa madiwani tunaomba mtuunge mkono ili bangi kwenye maeneo yetu iwe historia 


Mwl.Nchembe amesema ni vyema kila diwani akawa wakala wa wananchi anaowaongoza kwa kuwaelimisha na kuwaeleza jambo ambalo serikali italifanya halitokuwa na faida kwao isipokuwa ni hasara



Kwa upande wake mshauri wa jeshi la akiba Wilaya ya Arumeru Meja Hamis amesema jambo la kusikitisha  asilimia 90 ya wananchi wa Lesinoni Katabya Odonyowas na Kisimiri juu Kata ya Uwiro wanalima zao hiyo ambalo kisheria halitakiwi katika nchi ya Tanzania.


"Sisi madiwani ndiyo wenye watu lakini kuna baadhi ya madiwani hapa ukiwashika wanakuambia hao ni waiga kura wetu,kama mtu anavuta bangi kwa kawaida akili zake haziko vizuri na hata hii bajeti mnayoijadili ni kazi bure kama mnajadili na wananchi wenyewe ndiyo watumiaji wakuu wa madawa hayo ya kulevya."Alisema 


Ameongeza kuwa matumizi ya bangi ni sehemu ya maadui watatu ambao walizungumzwa na hayati baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere hivyo utokomezaji wa madawa hayo ya kulevya unawezekana pale tu kila mmoja atasimamia nafasi yake vyema.


"Haiwezekani mimi nakuja kufyeka bangi na wewe kiongozi upo,inasikitisha sana nilikuwa nasikia tu sasa nimejionea kwa macho na tukileta siasa bangi haiwezi ikaisha katika maeneo hayo na tusipoweza kuidhibiti ikiwa shambani ,ikisha vunwa hatutaweza kuidhibiti tena."Alisistiza Meja Hamis

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI