Teddy Kilanga_ARUSHA
Baadhi ya Wakazi wa jiji la Arusha wameiomba jiji la Arusha kuharakisha zoezi la anuani za makazi kwani linarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Wakizungumza baada ya kuona zoezi hilo katika mtaa wa majengo ulioka kata ya Levolosi jijini Arusha walisema zoezi hilo likikamilika litasaidia kutambua idadi ya makazi pamoja na kutambua wamiliki halisi wa maeneo yao.
Roman Abrahamu ni mmoja wa wakazi wa mtaa wa majengo ambapo alisema zoezi hilo likikamilika nchi itakaribiana na mataifa ya nje katika kurahisisha upatikanaji wa watu wanapoishi kupitia namba husika zinazotambulisha makazi.
"Hata kama ni mgeni anahitaji maelekezo ya mwenyeji wake anapoishi humpa urahisi wa kumwelekeza na kuelewa hivyo wananchi watoe ushirikiano kwa waendesha zoezi ili liweze kukamilika kwa wakati kwani lina faida kwetu na serikali pia,"alisema Abrahamu.
Naye Kaimu mtendaji wa kata ya Levolosi,Deliphina Loshohola alisema zoezi limeenda vizuri lakini ni vyema vijana watenda kazi wakaongezwa katika kusaidia zoezi hilo likaenda haraka angalau kuwe na kundi mbili au tatu kwa kila mtaa.
"Changamoto nyingine ni baadhi ya watu hawatoi ushirikiano katika kuonyesha namba zao kwani nyumba nyingi zilizopitiwa na mfumo wa awali unakuta namba hazipo hivyo inabidi kuuliza wenyeji wanashindwa kutoa ushirikiano wa kutosha,"alisema Kaimu huyo Mtendaji wa kata ya Levolosi.
Joshua Shango ni mmoja wa wasajili wa anwani za makazi ambapo alisema hadi sasa wameshapitia nyumba zaidi ya 53 katika mtaa wa majengo hivyo zoezi limeenda vizuri na watajitahidi kumaliza kwa wakati.
Mratibu wa zoezi hilo la ukusanyaji taarifa za anwani za makazi katika kata ya Levolosi,Haliye Abubakari alisema zoezi hilo limeenda vizuri kutokana na hapo awali lilikuwa limeshafanyiwa kazi katika kata hiyo.
"Sasa hivi zoezi tunalolifanya ni kuhakiki vile vibao vya namba kama vipo na kama havipo wanaanza kuhesabu upya kwani hadi sasa kwenye mtaa huo wamefikia kata tatu hivyo tunategemea zoezi hili kukamilika ndani ya siku tatu,"alisema.
0 Comments