Na Hamida Ramadhan Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Sulemani Jafo amesema kuwa Athari za uharibifu wa mazingira zimesababisha ukame na kupelekea nchi kuingia katika mgao wa maji na umeme.
Amesema ukame huo umepelekea athari ya kiuchumi kwani wakulima walishindwa kuzalisha mazao kipato kikashuka wafugaji walipoteza mifugo kipato kikashuka pia maji yalishindwa kutililika kilimo cha umwagiliaji kikashindikana na hata mabwawa yanayotumia maji kuzalisha umeme ilichindikana na kupeleka umeme kuwa mdogo.
Hakiongea wakati wa uzinduzi wa Bodi ya baraza la Uhifadhi wa Mazingira Nchini (NEMC) Waziri huyo amesema kuwa kutokana na hayo ajenda ya Mazingira ni Muhimu kwa mstakabali wa taifa lakini pia ameeleza ajenda hiyo ni ya kidunia.
" Nikuweli usiopingika bila kusimamia vizuri suala la Mazingira dunia itakuwa katika changamoto kubwa na ndio maana dunia yote kwa umoja inajadili suala zima la mazingira na ndio maana hata katika mikutano ya Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa dira ya taifa katika upande wa Mazingira," amesema Waziri Jafo.
Amesema katika siku za hivi karibuni tulisikia keleke nyingi watu wakilalamika mgao wa maji hasa katika mkoa wa Dar es Salaam.
"Katika miezi michache kabla ya mvua kunyesha maji yalikuwa machache tumeona uhaba wa maji ulikuwa mkubwa kupita kiasi ni kwasababu vyanzo vya maji vingi vilikuwa vikitililisha maji chini ya chini ya uwezo na kuoelekea mgao wa maji kwa baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam huku wanyama wakifa yote ni mbadailiko ya tabia nchi .
"Leo hii tunapo zindua bodi hii ambalo jukumu lake kubwa ni kwenda kusimamia masuala mazima ya Mazingira NEMC tunaimani kuwa mtakwenda kufanya vizuri kama matarajio yetu muende mkafanye kazi kwa ubora zaidi ili nchi yetu iweze kusonga mbele," amesema
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga amempongeza Mwenyekiti Prof. Esnati Chaggu na wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuongoza Taasisi hiyo yenye jukumu kubwa la kusimamia masuala ya mazingira Nchini.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa Bodi, Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Profesa Mhandisi Chaggu amesema wana dhamana kubwa katika kuhakikisha agenda ya mazingira inapewa msukumo wa dhati kwa kuwa ni mjadala wa dunia kwa sasa.
0 Comments