MWANZA.
Mfuko wa Mawasiliano kwa wote yakutana na wadau wanaotoa huduma za mawasiliano kanda ya ziwa na kutoa elimu.
Fredy Kandongo Afisa Sheria kutoka Mfuko wa Masiliano kwa Wote ameeleza kuwa lengo la elimu hiyo ni kuendeleza kutoa elimu kwa watoa huduma za mawasiliano na wadau wengine ili kuweza kufahamu mfuko huo, kazi wanazofanya, kutoa mrejesho wa kazi walizofanya kwa kipindi husika na kupata maoni kutoka kwa watoa huduma na kuona namna gani wanaweza kushirikiana nao kuboresha kazi na kutoa huduma bora kwa watanzania ili waweze kunufaika.
"Kimsingi watoa huduma hii ni watu wa msingi sana katika kuhakikisha watanzania popote pale walipo wananufaika hususani walipo kanda ya ziwa wanapata huduma za mawasiliano ya uhakika" Alisema Fredy.
Fredy ameeleza kuwa kwa sasa wana kata takribani 1000 za mawasiliano ya simu ambapo kata mia 700 zimeishakamilika na kata 300 ziko katika hatua mbalimbali.
"Sasa hivi tumeenda hatua za mbele zaidi kwamba tutakuwa tunajenga minara ya kurushia matangazo ya radio" Alisema Fredy.
Aidha ameongeza kuwa kazi hiyo wataifanya kwa kushirikiana na Halmashauri ambapo zitawajibika kuanisha maeneo ambayo kimsingi yanahuduma na yasio kuwa na huduma.
Kwa upande wake Mkurungenzi wa TCRA Kanda ya Ziwa mhandisi Francis Mihayo ameeleza kuwa watahakikisha maeneo yote ya kanda ya ziwa yanapata radio ili wananchi kupata urahisi wa kupata habari.
"Ukienda sehemu zingine hazina kabisa radio hususani maeneo ya mipakani, wanahitaji kupata radio za uhakika ambazo zinatolewa katika nchi yetu" Alisema Mihayo.
Mihayo ameeleza kuwa badala ya watu wa mipakani kusikiliza radio za mipakani bado nafasi za kuanzisha redio zipo na kufanya hivyo watawasaidia watu hao kuelewa nini kinaendelea katika nchi yao.
" Bahati nzuri serikali yetu imepunguza gharama za uanziashaji wa redio tofauti na kipindi cha nyuma waliogopa gharama za uanzishaji wa redio pamoja na gharama za mwaka sasa hivi ziko chini ni kuwasiliana na mamlaka ya mawasiliano ili kupata maelekezo namna ya kuanzisha" Alisema Mihayo.
Ameeleza kuwa kuanzishwa kwa radio mipakani watu wanaoishi huku wataweza kupata taarifa kwa wakati kuelewa taratibu za maeneo yao pamoja kupata taatifa za viongozi wa serikali kwa wakati.
0 Comments