Header Ads Widget

TAARIFA KUHUSU TUKIO LA MOTO BENK YA NMB IRINGA








MJI  wa  Iringa   Leo umekubwa na taharuki   kubwa baada ya  tukio la  moto  kutokea  katika  benk ya  NMB tawi la Mkwawa  huku  kamanda  wa polisi  mkoa wa Iringa wa  Iringa Allan Bukumbi akisema kwenye  tukio  hilo wafanyakazi  watatu wa benki  hiyo  wamejeruhiwa na  kukimbizwa katika Haspitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa .

Baadhi ya  wateja  wa  benki  hiyo  waliokuwepo  wakati moto  huo ukianza  kuwaka  walisema   walipatwa na mshituko  mkubwa baada ya  kutokea  kwa  tukio  hilo huku magari ya zimamoto na uokoaji  yakiwa  nje ya  jengo hilo  na  kuanza  kupambana  kuzima  moto  huo .

Alisema  mteja  Godlove  Yona  kuwa  akiwa katika  foleni ya  kuhudumiwa  alisikia  wafanyakazi wa  benki  hiyo  wakiwataka  wateja  kukimbia nje ya  jengo kwani  hali ya  hatari  imejitokeza  kwa  moto  kuanza  kuwa ndani ya jengo  hilo .

Akizungumza na waandishi  wa habari    juu ya  tukio  hilo kamanda Bukumbi  alisema  kuwa  kutokana na  tukio  hilo ni  watu  watatu  wamejeruhiwa na kuwa  kuhusu  suala la usalama wa mali za  benki  hiyo hadi sasa hakuna upotevu  wa  fedha zaidi ya  kuwepo kwa  uharibifu kiasi katika  chumba cha mkutano ambako  moto  huo ulianzia.

Kamanda  Bukumbi mbali ya  askari wa  jeshi la  polisi  kufika kwa wakati  eneo hilo pia amewapongeza  wafanyakazi wa  benki ya  NMB   tawi la Mkwawa ,jeshi la zimamoto na uokoaji  kwa  kufika kwa wakati  eneo hilo  kusaidia  kuthibiti  moto  huo  .

Aidha  aliwataka  wananchi  kuendelea  kuchukua  tahadhari  hasa  yanapotokea matukio ya  hatari kama  ya moto na mengine  kuacha kukimbilia sehemu ya  tukio  kwani ni hatari kwa  usalama  wao.

Meneja  wa Benki ya  NMB  Iringa  Colman Kiwia  alisema  kuwa  tukio hilo la moto lilikuwa ni zoezi la utayari  wa majanga ya  moto  kwa  mujibu wa  sheria ya  usalama kazini inayowataka  kufanya   hivyo na benki  hiyo kwa  mujibu wa  sheria ya   usalama maeneo ya kazi na  kuwa  tukio  hilo  si halisi  kwani  limefanywa kama  sehemu ya kutimiza  matakwa ya  kisheria  ya sheria  za usalama sehemu za kazi .


" Niwaambie  tu  majanga ya  moto hayaepukiki  lakini  tunaweza  kuchukua tahadhari ya majanga  haya ya  moto  kwa  kukata bima  za majanga kuepuka hasara ambapo  benki ya  NMB tumekuwa  tukitoa  huduma ya  bima   hiyo  na nyingine  kama  magari ,vifo na elimu  bima  zote  zinatolewa  pamoja na mambo mengine  tunatoa mikopo  ya  kilimo ,  biashara na  tuna ofa maalumu ya Uwekezaji Amana kwenye akaunti ya JASIRI bundi inayoishia tarehe  21 Machi "

 Kamanda  wa  jeshi la zimamoto na uokoaji  mkoa wa Iringa Isabela Mbwago  alisema  kuwa  wananchi  wanapaswa  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa  jeshi   hilo kwa  kupiga namba  114  pindi yanapotokea majanga ya moto japo  alitoa angalizo ya  matumizi sahihi ya namba  hiyo .




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI