Header Ads Widget

RUVU SHOOTING KUKIPIGA KESHO DHIDI YA DODOMA JIJI KESHO

 



TIMU za Soka za Ruvu Shooting ya Kibaha Mkoani Pwani kesho Jumapili inatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaofanyika kwenye uwanja wa Mabatini Ruvu Mlandizi.


Aidha katika mchezo huo washabiki 20 wa kwanza watakaopata chanjo ya Covid-19 wataingia bure uwanjani huku elimu ya kujikinga na ugonjwa huo ikitolewa uwanjani hapo.


Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja huo manahodha wa timu hizo pamoja na walimu wasaidizi wa timu hizo kila moja wamejinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo.


Wenyeji wa mchezo huo kupitia Mwalimu msaidizi wa Ruvu Shooting Rajab Nakuchema alisema licha ya mchezo huo kuwa mgumu lakini watatumia vyema uwanja wao wa nyumbani kupata alama tatu ambazo kwao ni muhimu.


Nakuchema alisema kuwa licha ya kufanya vibaya kidogo kwenye baadhi ya michezo lakini kufuatia usajili wa dirisha dogo wamesajili wachezaji wazuri hivyo kufanya vizuri katika hatua hii inayofuata ambapo walifanya vibaya kutokana na baadhi ya wachezaji wao kuwa mafunzoni.



Kwa upande wake nahodha wa Ruvu Shooting Renatus Kisase alisema kwa sasa wako vizuri na watafanya vizuri kwenye uwanja wao wa nyumbani ambao hawajautumia kwa muda kupisha marekebisho.


Naye Mwalimu Mohamed Muya alisema kuwa anatarajia mchezo huo kuwa mgumu lakini wana uhakika wa ushindi kwani ushindi kwao utawaweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI