Header Ads Widget

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA CHUO CHA CCM

 


RC  Abubakari Kunenge

 

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Chuo Cha Uongozi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM).


 Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Februari 23 ambapo Rais ndiye atakayekizindua.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema chuo hicho kinaendeshwa kwa pamoja na vyama vya ukombozi Kusini mwa Afrika.


Alisema kuwa vyama hivyo ni vyama rafiki na CCM vitawakilishwa na makatibu wakuu wa vyama hivyo. 


"Siku moja kabla ya uzinduzi huo katibu mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo atazindua barabara ya lami yenye urefu wa kilometa mbili kuelekea kwenye chuo hicho,"alisema Kunenge.


Aidha alisema kuwa kwenye uzinduzi wa barabara hiyo makatibu wakuu wa vyama hivyo rafiki watashiriki.


Alivitaja vyama hivyo kuwa ni ZANU PF cha Zimbabwe, MPLA cha Angola, SWAPO Namibia FRELIMO Msumbiji na ANC Afrika Kusini.


Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo na kumuunga mkono Rais.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI