Header Ads Widget

RADI YAUWA MMOJA NA KUJERUHI WANNE LINDI

 



NA HADIJA OMARY LINDI......


Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa katika maeneo yao ya biashara wakiuza mkaa  pembezoni mwa barabara ya Kiwawa Wilayani kilwa Mkoani Lindi 



Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi. Matiro Kitinkwi ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea tarehe   04/02/2022 Majira ya  Saa 17:30hrs huko kitongoji cha  Kiukula Kijiji Cha Kiwawa Wilayani Kilwa



Kamanda Kitinkwi Alisema katika tukio hilo mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Jackson Yohana  (28) Mkulima na Mkazi wa Morogoro Alifariki dunia huku  Saidi Naulungu (34) mkazi wa kiwawa alipata mchubuko mkono wa kulia , Selemani Mikidadi (27)  Mkazi wa Kiwawa-Amepata mchubuko mdomoni   ambapo Mohamed Nauluku (42)  Mkazi wa Kiwawa poja na  SAID KIBINI (50)  Mkazi wa Kiwawa wamelazwa katika hopitali ya wilaya ya Kinyonga Hospital 



Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa hospital ya Wilaya ya kilwa Kinyonga Dokta Mocha alithibitisha kupokea majiruhi wawili wakitokea katika kituo cha afya kiwawa



" ni kweli hilo tukio limetokea katika eneo la kiwawa kwamba watu watano wamepigwa na radi na mmoja kufariki papo hapo kati yao wawili walitibiwa katika kituo cha afya kiwawa na wengine wawili waliletwa hapa kwa matibabu zaidi"



"Walivyoletwa hapa baada ya vipimo tuligundua walipata mshituko wa kawaida ambao uliwapelekea kupoteza fahamu ambapo mmoja alikuwa anashindwa kumeza tumewapatia matibabu na sasa wanaendelea vizuri " alifafanua Dokta Mocha



Mw

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI