Header Ads Widget

MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA MICHIGAN NCHINI MAREKANI ATEULIWA KUWA BALOZI WA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

 




Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani ili kuongeza idadi ya watalii wanaotoka nchini Marekani  


Hatua hiyo ni inakuja ikiwa ni jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii  kuanza kuteka soko endelevu la Utalii la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Marekani hususan vilivyopo katika Jimbo la Michigan 


Akizungumza hivi karibuni kwenye ziara ya kikazi katika mji wa Detroit nchini Marekani Waziri Ndumbaro amesema  amelazimika kumteua Balozi huyo kutokana na ushawishi wake mkubwa  katika jamii na pia Prof. Julian ni zao la Tanzania


Amesema  Prof. Juliani  amezaliwa nchini Marekani lakini amesoma  katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia amekaa Tanzania kwa  zaidi ya  miaka 15


Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema Prof. Julian mbali ya kuwa Mwenyeji nchini Tanzania bali ni mtu mahiri anayezungumza lugha ya kiswahili ya ufasaha wa hali ya juu.


Amesema anaamini  atakuwa  Balozi mzuri wa utalii wa Tanzania kwa sababu maeneo mengi ya utalii anayajua hususani maeneo ya kusini ambako alitumia muda mwingi katika maeneo  hayo kufanya utafiti.



“ Uteuzi wake sio wa kubahatisha ni mtu ambaye amekuwa anaipenda sana nchi ya  Tanzania na amekuwa muumini mkubwa wa utalii wa utamaduni hivyo atakuwa chachu kwa Wanafunzi anaowafundisha kuwachochea kuja nchini Tanzania na hili ndo soko tunalolitaka kwa sasa'' amesisitiza Dkt, Ndumbaro

Wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kukuza utalii kwa kuongeza watalii kutoka Marekani 


Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, takwimu za mwaka 2020/2021 zinaonyesha Marekani ilikuwa ya tano kwa idadi ya watalii  waliotembelea Tanzania huku Uingereza ikiwa ya 16.


Kwa upande wake, Prof. Julian amesema kuwa yeye atakuwa balozi mzuri katika kutangaza mazuri ya Tanzania na utalii wake duniani kote hasa kwa wanafunzi anaowafundisha na pia kwa jamii yote inayomzunguka



“Kila nitakapopata fursa nitawaambia kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wakarimu sana, nitazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania na nitawaeleza sehemu mahsusi za kitalii zilizoko Tanzania.


Hata hivyo, Prof. Julian amesema hata kabla ya kuteuliwa amekuwa mstari wa mbele kutangaza vivutio vya utalii katika kazi yake anayoifanya ya kufundisha wanafunzi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI