Header Ads Widget

MARAFIKI WA SERENGETI WAKABIDHI GARI TANAPA KWA AJILI YA ULINZI WA FARU SERENGETI

 


Na Edmund Salaho.TANAPA


Taasisi ya Marafiki wa Serengeti Tanzania (Friends of Serengeti Tanzania ) wamekabidhi gari aina ya Toyota landcruiser pickup lenye thamani ya shillingi millioni 69,  kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ambalo litatumika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa Faru katika eneo la Moru.

 

Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha katika Makao Makuu ya shirika hilo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Marafiki wa Serengeti Tanzania Suzan Shio  alikabidhi gari hilo kwa Kamishna wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi Martin Loibooki ambaye naye alikabidhi kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Masana Mwishawa.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Shio amesema msada huo ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na taasisi hiyo katika hifadhi za taifa za Tanzania kwa lengo la kusaidia uhifadhi.

 


“leo tunakabidhi gari hili ambalo litasaidia uhifadhi wa faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti  katika eneo la Moru ingawa kwa miaka mingi marafiki wa Serengeti tumekuwa tukisaidia Hifadhi za Taifa za Serengeti na Tarangire ”,alisema Shio.



Shio amesema Marafiki wa Serengeti wamefanya vitu vingi katika hifadhi hizo ikiwemo ujenzi wa vituo vya maaskari vinne,katika hifadhi ya Tarangie,vituo vya askari vinne katika hifadhi ya Serengeti na misada mingine .


Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Kamishna wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi Martin Loibooki ameishukuru Taasisi ya Marafiki wa Serengeti kwa kwa msaada wa gari hilo ambalo litakwenda kuimarisha ulinzi katika hifadhi ya Serengeti  ambalo ni litaongeza jitihada za ulinzi wa Faru.

 


“Napenda kusimama hapa kupokea gari aina ya Toyota land cruiser ambalo limetolewa na wahisani wa shirika la marafiki wa Serengeti ambalo wamelitoa kwa ajili hifadhi hii ambapo tunaahidi kulitumia gari hili kwa malengo yaliyokusudiwa” alisema Loiboki

 

Kamishna Loibooki amesema TANAPA inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi ya Marafiki wa Serengeti ambao tangu mwaka 1984 limekuwa likitekeleza miradi mingi katika hifadhi za taifa za Tarangire,Serengeti na hifadhi nyingine za taifa

 

 

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Masana Mwishawa ambaye ni Mkuu wa  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ameshukuru taasisi ya Marafiki wa Serengeti kwa kutoa  gari hilo hilo na kuahidi kulitumia kwenye kuinarisha ulinzi wa wanyama adimu jamii ya faru katika hifadhi hiyo.

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI