Katika kuelekea maandalizi ya ya mashindano ya michezo ya umitashumita na umiseta manispaa ya Moshi Diwani wa kata ya Kiborloni Frenki Kagoma ametoa msaada wa vifaa vya michezo kwa shule ya secondari ya Kiborloni ili kuwawezesha wanafunzi hao kushiriki vyema na kushinda katika michezo hiyo.Mwandishi Rehema Abraham , MDTV Kilimanjaro
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhi vifaa hivyo vya michezo ambazo zilienda sanjari na uzinduzi wa mashindano ya Kagoma CUP amesema vifaa hivyo vitawasaidia uboreshaji wa elimu na suala Zima la michezo Mashuleni huku akiwataka wadau wengine kujitokeza na kitaatua changamoto mbalimbali zinazoikabili secta ya michezo Mashuleni.
Sambamba na hayo amesema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ya ligi ya Kagoma CUP ni kuongeza Chachu ya kusoma kwa wanafunzi wawe na hari ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Amesema kuwa katika ligi mbalimbali zinazorndeshwa ndiko kunakoibuliwa vipaji na pia wachezaji Bora wa kimataifa huanzia ngazi ya chini mpaka Wanapofika kwenye timu za juu.
"Tutegemee mafanikio kwani hata timu nyingine zinaweza kuona wachezaji kwenye timu maana bà ada ya muda viwango vyao vitakuwa vimepanda "Alisema Kagoma.
Hata hivyo Amesema kuwa atatoa zawadi kwa washindi mbalimbali watakaoshinda mashindano hayo ambao ni mchezaji boraa, mfungaji Bora ,timu yenye nidhamu .
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo ya Kiborloni Philipo Simon amemuomba diwani huyo kusaidia kutatua changamoto ya viwanja kwani viwanja wanavyovitumia wanafunzi vinakuwa katika hali isiyoridhisha .
"Ukiangalia uwanja wetu kuna mifereji kuna vumbi, lakini kwa kupitia mashindano haya una nguvu ya kuweza kutupatia wafadhili wakaweza kututengenezea uwanja "Alisema.
Hata hivyo Amesema kuwa Wana uhaba wa vifaa vya michezo ambayo imekuwa changamoto kwa muda lakini wanaendelea kutatua mwaka hadi mwaka.
0 Comments