Header Ads Widget

ASKARI 11 WA JESHI LA MAGEREZA KANDA YA KASKAZINI WATUNUKIWA NISHANI MBALIMBALI

Askari 11wa jeshi la magereza Kanda ya kaskazini wametunukiwa nishani mbalimbali katika hafla ya iliyofanyika viwanja vya gereza la karanga wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro .Mwandishi wa Matukio Daima  Rehema Abraham anaripoti 


Akiwatunuku nishani hizo Kamishna  Jenerali wa jeshi la magereza nchini (CGP ) major Generali Suleiman Mungia Mzee amesema kuwa kila askari anapotunukiwa nishani ansonesha furaha kwani inaonesha utumishi wake katika jeshi umethaminiwa na uongozi.


"Lakini pia ni mda mrefu hatujapata hizi nishani kwa hiyo kwa kipekee kabisa nitumie pia fursa hii kumshukuru Mh Raisi Samia Suluhu Hasan kwa mambo makubwa mawili,ametupatia vyeo vya kutosha,lakini akaona haitoshi ametupatia nishani za kutosha kwa hiyo kwa ujumla tunaendelea kutekeleza utaratibu wa kuewavalisha ,tumeshaanza dar es salaam na Sasa hivi tunamaliza Kanda ya kaskazini na tumebakiza Kanda ya kati"Alisema.



Hata hivyo amewataka Askari wote waliotunukiwa nishani kujua kwamba utendaji wao uliotukuka umeonekana hivyo wasibweteke kwa kupata nishani hizo Bali waone Wana wajibu wa kufanya zaidi ya walivyofanya ili waweze kupata matunda mengine kutoka katika Serikali .


Naye Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amewapongeza askari hao wa jeshi la magereza kwa kutunukiwa nishani hizo na kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa mstakabadhi wa nchi yetu .


Sambamba na hayo amewaomba askari hao kuiamini Serikali kwani na wao wameaminiwa na wasomwangushe Mh.Raisi kwa kufanya au kukiuka Sheria.


Hata hivyo amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama  kuungana kwa pamoja na kufanya utafiti wa mauji yansyoendelea hapa nchini ili kujua tatizo liko wapi na liweze kupatiwa ufumbuzi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI