Header Ads Widget

WAZIRI NDUMBARO AMPONGEZA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI, ATAKA KUKUA KWA DIPLOMASIA YA UCHUMI KATIKA UTALII

 


 


NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK, MAREKANI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuweka nguvu za kutosha  katika kufanya Diplomasia ya Uchumi ikiwemo kuwavutia watalii kutoka nje ya nchi kuja nchini.


Ametoa kauli hiyo leo wakati mara baada ya kufanya ziara ya  kutembelea ofisi ya Ubalozi huo ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na Watumishi na Wawekezaji mara baada ya kumalizika kufanyika kwa mkutano wa 50 wa mwaka wa uwindaji wa kitalii uliofanyika katika Jiji la Las Vegas nchini Mareakani.


Akizungumza na timu ya Watumishi hao, Dkt. Ndumbaro amempongeza Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza kwa kazi kubwa anayoifanya ya Diplomasia katika tasni ya biashara na utalii.


Ambapo amewataka Wanadiplomasia hao kuwa daraja katika  kuwawezesha watalii kuja  nchini Tanzania 


Amesema Diplomasia ya uchumi katika tasnia ya utalii, Wanadiplomasia hao wanapaswa  kutangaza na kujibu maswali ya watu mbalimbali wanaotaka kutalii Tanzania kuhusu namna ya kufika nchini kiujumla na katika kila kivutio cha utalii kimahususi.


"Kutokana na kasi kubwa ya maendeleo ya kiuchumi, Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi Diplomasia ya kiuchumi ndo injini ya maendeleo haikwepi, ongezeni ujuzi katika eneo hilo." amesisitiza Dkt. Ndumbaro.


Aidha, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi hao kuwa mstari wa mbele katika kujua masuala ya uwekezaji na biashara pamoja na mambo yote muhimu kuhusu utalii nchini ili waweze kuwaelezea wananchi wanaowahudumia


Vilevile amewataka   kusababisha watalii kutoka katika nchi waliyopo kuhudhuria katika mikutano, makongamano na maonyesho ya utalii ya ndani ya Tanzania ikiwemo 

matamasha ya kiutamaduni .


Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amempongeza na kumwalika nchini Tanzania, Kiongozi wa Vyama vya Waongoza Watalii nchini Marekani, Rumit Mehta kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko Ukanda wa Kusini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI