Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wao mapema shuleni ili kuwaandishika kwa ajili ya kuaza shule ifikapo January 17 mwaka 2022 Ili kuepuka usumbufu.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa Shaaban Maliyatabu wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa madarasa 12 ya Sekondari ya Bonyokwa yaliojengwa kwa ajili ya pesa za Uviko 19.
Aidha, amesema kuwa madarasa hayo yamekamilika kwa ajili ya mtoto kuanza kusoma hivyo, ni vyema wazazi kuwapeleka watoto wao kwa ajili ya kupata elimu ambayo itawasaidia katika maisha yao.
Hata hivyo, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa kwa ajili ya kujenga madarasa hayo 12 ambayo yanakwenda kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa darasa moja wanafunzi wengi zaidi.
Amesema kuwa, ni vyema wazazi kuwapeleka watoto wao mapema shule Ili kuanza masomo tarehe 17, mwezi wa kwanza mwaka huu kwa ajili ya kuanza masomo .
Hata hivyo, amewashuruku viongozi wote walioshiriki kwa namna moja na nyengine katika kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo ambayo yamekua mkombozi wa changamoto iliyokuepo kwa muda mrefu.
"Uongozi wa Serikali ya mtaa ya Bonyokwa tunatoa shukurani za dhati kwa Rais wetu mpemdwa pamoja na viongozi wote akiwemo Mkurugenzi wa jiji mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Meya, Mbunge Jimbo la Segerea na Diwani wa Bonyokwa"amesema Maliyatabu.
Katika hatua nyengine,amewataka wananchi kushiriki kwa pamoja shughuli za maendeleo Ili kuleta matokeo chanya katika jamii.
0 Comments