Idara ya uhamiaji mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama siku ya jumatano tarehe 12, 2022 majira ya saa 11 jioni imefanikiwa kuwakata wahamiaji haramu wapatao 40 raia wa Ethiopia.Mwandishi Zacharia Nyamoga,Matukio Daima Iringa
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa uhamiaji Mkoa wa Iringa Agnes Luziga amesema wahamiaji hao walikamatwa katika gari aina ya fuso yenye usajili namba T-517 DJY mali ya Deogratius Kimambo raia wa Kilimanjaro likiwa limetelekezwa barabara ya Iringa – Mbeya
Akifafanua zaidi Agnes Luziga amesema baada ya upekuzi walifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wapatao 40 wakitokea Ethiopia kuelekea Afrika ya Kusini.
Aidha Agnes Luziga amesema wanaendelea na taratibu za kimahakama na watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo januari 13, 2022
Ameongeza kwa kutoa lai kwa Watanzania kutoa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo karibu kwa kufichua pale wanapo waona watu ambao wanawatilia mashaka.
“Tunashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichuwa hawa waharifu tunashirikiana kwa kupashana habari kama kuna matukio kama haya ili waletwe katika sehemu husika pia huwa tunatoa elimu katika redio kwa wananchi kuwa wanapo waona watu wanao watilia mashaka basi watoe taarifa ofisi au kwenye chombo chochote cha ulinzi na usalama kilichopo karibu” Amesema Agnes Luziga
Kwa upande mwingine kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP - Allan Bukumbi akijibu kuhusu usalama mkoa wa Iringa kamanda amesema wahamiaji hao hawajahatarisha hali ya usalama kwasababu walikuwa wakipita tu kutoka Ethiopia kwenda Afrika ya kusini.
Pia ACP-Allan Bukumbi ameongeza kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa ujangili wakiwa na pembe za ndovu zenye zenye uzito wa kilogram 66.5 zenye thamani ya zaidi milioni mia mbili za Kitanzania.
0 Comments