Adeladius Makwega_Dodoma.
Wajita na Wakerewe wamekuwa na utani mkubwa kwa muda mrefu, hilo linatokana na mila na tamaduni kadhaa zinazowazunguka makabila haya mawili kama nilivyoeleza katika matini yangu ya kwanza ya Utani wa Wajita na Wakerewe. Japokuwa baadaye mambo haya yamebadilika kwa sababu mbalimbali ikiwamo kwa kuingia kwa Ukristo katika eneo hilo.
Kwa kutazama leo baadhi ya tamaduni ziweza kutazwa kuwa ni hasi au chanya, lakini kutakana na kubadilika kwa jamii na kuingia kwa tamaduni mpya baadhi ya wazaliwa wa sasa hawezi kuamini kuwa haya mambo yapo au yalikuwapo katika jamii zao.
Wajita walikuwa na mtazamo kuwa wanawake wa Wakerewe ni wahuni sana, wanaamini hivyo kutokana na sababu mbalimbali.
“Kwanza, binti wa Kikerewe akiwa tu na umri wa miaka 12 alikuwa akifundishwa tabia ya kuzivuta sehemu zake za siri kila mara na jambo hilo lilifanya wanawake wa Kikerewe kuwa na kiungo hicho kuwa na urefu hata kwa inchi tano. Jambo hilo likiaminika kuwa waliweza kufuraia zaidi tendo la ndoa.” Haya yanathibitihswa na G.S. Gasase katika andiko lake juu Utani Relatioship in Jita.
Ndugu Gasase ambaye alikwenda mbali zaidi akisema kuwa kabla mwanaume hajamuingilia mwanamke huyo kwa mila za Wakerewe basi huwa na wajibu wa kushikwa kiungo hicho na jambo hilo lilimsisimua mno . Kulingana mila’ za Wanaume Wakerewe mwanamke ambaye hana kiungo hicho kirefu havutii kimapenzi.
Lakini huku Wajita wakiwatania Wakerewe kuwa makahaba kwa kuwa na kiungo hicho kirefu. Kwa hilo naweza kusema ndiyo maana makabila mengi yalisisitiza kuoana wenyewe kwa wenyewe ili kuweza kuficha baadhi ya mambo ya makabila yao na yasijulikana na makabila mengine.
Swali ubaoni, je kukutaza kuoa kabila lingine lilikuwa kosa? Msomaji wa matini hii nadhani jibu lako unalo moyoni mwako.
Kulingana na mila za Kikerewe mwanamke harusiwi kula nyama ya mbuzi, kuku na samaki wakubwa hivyo ni vyakula vya wanaume tu. Jambo hilo linafanywa wanaume wanapokula vyakula hivyo huwa hawasumbiliwi na wanawake wa Kikerewe. Nao linawafanya Wajita kuzidi kuwazodoa Wakerewe na kuwacheka kuwa wanaume wao kujipembelea zaidi ya wanawake wao.
Pia Wakerewe lilikuwa kabila ambalo halifanyi tohara ya wanaume, kwa hiyo Wajita walikuwa wakiwatania Wakerewe kuwa mwanamke wa Kijita hawezi kutembea na mwanamme Mkerewe kwa kuwa hajafanya tohara.
Hoja hii ya uchafu pia inatazamwa hadi katika chakula kwani Wajita walikuwa wanasema kuwa hawezi kula chakula pamoja naWakerewe kwa kuwa hawajakwenda jandoni.
Wakerewe wamekuwa na hoja nzito dhidi ya tohara hiyo ya wanaume wakidai kuwa kwanini kiungo hicho kimeumbwa hivyo? Mungu angeweza kukiumba vinginevyo, kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maamuzi ya aliyetuumba, huku inapobainika kuwa mwanaume huyo kafanyiwa hivyo aliweza kuinyimwa majukumu yoyote ya jamii hiyo hata uongozi.
Mwanakwetu kwa leo naishia hapo, hao ndiyo ya Wajita na watani zao. Nahakika ndugu yangu msomaji wa matini hizo unaweza kuwa na maswali ya kuniuliza kwa nambari na barua pepe hapo chini na mimi kuyatafuta majibu hayo iwe kutoka kwangu mimi au wale waliofanya tafiti juu ya makabila haya au wazee wa makabila haya.
Hayo yote niliyokusimulia yanawezekana leo hii yakawa sivyo kutokana na sheria, mila kubadilika kwa mambo na nakadhalika lakini kwa ukweli Mungu ndivyo hali ilivyokuwa. Nakutakia siku njema
makwadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments