Header Ads Widget

NSS YAZINDUA MICHUANO YA MPIRA WA MIGUU

 



Wadau mbalimbali nchini Tanzania wametakiwa kujitokeza kudhamini mashindando ya mpira wa miguu yanayojulikana kama After School Clash yalioandaliwa na Taasisi ya ukuzaji michezo (Mass Sport Solution (NSS)..............Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam



Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Nassor Mungaya wakati akizindua mashindano hayo ambapo amesema lengo ni kukuza michezo, huku timu nane zitashiriki kutoka shule mbalimbali.


Amesema kuwa,  michuano hiyo itakuwa ni maalum kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita ambao wamehitimu masomo yao na kusubiri matokeo Ili waweze kujiendeleza na masomo yao, huku akiahidi kuipeleka nchi nzima.


Akitaka shule zitazoshiriki michuano hiyo kwa sasa ni pamoja na Alpha Secondary Ahmes Secondary, Crown Secondary, Marian Boys sec,Rosmin Secondary, ST Joseph Boys Secondary, Heritage Secondary pamoja na Shule ya Wavulana ya Abbey Secondari.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI