Waziri wa madini Mhe. Dotto Biteko amewataka wachimbaji wakubwa na wadogo kuacha kutengeneza migogoro katika machimbo ya madini ili migodi hiyo iwanufaishe .
Biteko ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na wachimbaji wakubwa ba wagodo wa madini ya Dhahabu katika Kijiji Cha Mazizi kata ya Maseyu Wilaya ya Morogoro.
Anasema kuwa kumekua na tabia ya baadhi ya wachimbaji kutengeneza migogoro katika machimbo kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo na pato la Taifa.
Katika hatua nyingine waziri Biteko amempongeza Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Mazingira rafiki ya uwekezaji katika sekta hiyo.
Biteko anasema kitendo cha Rais Samia kusafiri nje ya nchi kimesaidia kuongeza wawekezaji ambao walikua wakiogopa kuja kuwekeza kwa sababu mbalimbali.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema atahakikisha machimbo hayo yanawanufaisha wachimbaji wa eneo Hilo badala ya kuwanufaisha wageni pekee.
Msando anasema licha ya kuwepo na wachimbaji wakubwa lakini lazima na wakazi wa eneo Hilo wanufaike kutokana na madini hayo kwa kuhakikiksha wawekezaji hao wanachangia shughuli za maendeleo
0 Comments