Na, Titus Mwombeki-MTDTV KAGERA.
Kamati aliyoundwa na mkuu wa Wilaya ya Bukoba kwa maagizo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kagera baada ya kupata fununuza za kuwepo kwa ufujaji wa fedha za umma unaofanywa na baadhi ya viongozi wasio waadilifu katika kitengo cha ukusanyaji mapato kwenye halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imebaini kuwepo kwa upotevu wa zaidi ya shilingi mil.300.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkoa huo uliopo Manispaa ya Bukoba baada ya kikao na wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo ili kujadili ripoti iliyoletwa na kamati ya uchunguzi dhidi ya sakata hilo.
“ Kamati hiyo ilipotia nyaraka mbalimbali zinazohusiana na ofisi ya afisa biashara wa halmashauri ya Bukoba mijini, tulianza na kitengo kimoja cha ukaguzi na utoaji wa leseni za biashara kama ‘sample’ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba mjini,uchunguzi ulifanyika katika nyakati tofauti tofauti na kubaini ubadhirifu wa fedha nyingi zilizoingia mifukoni mwa baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu katika kitengo cha utoaji wa lesseni tu, kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2021ndicho kipindi ambacho ubadhurifu ulikuwa kidogo zaidi na hii nikwasababu nilimsimamisha kazi afisa biashara wa halmashauri ya Bukoba mjini, fedha hizi ni nyingi zingesaidia kusogeza maendeleo katika mkoa wetu wa kagera”
Aidha, ameongeza kuwa kamati hiyo pia iliweza kubaini aina mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na watendaji katika kitengo cha utoaji wa reseni kwenye halmashauri hiyo ili kujinufaisha wenyewe.
“Kwa Mfano,Kuna kampuni ya utafiti iitwayo E.D.I limited kampuni hii ilipewa leseni namba B.03292344 kwa kulipa fedha katika kipindi cha mwaka 2020/2021 zaidi ya shilingi mil.4 lakini kwenye mfumo unaotumika katika makusanyo ya fedha ndani ya halmashauri ya Bukoba mjini inasomeka hakuna hata shilingi moja iliyowekwa na udanganyifu mwingine uliokuwa unatokea pale mfanya biashara anapokwenda kulipia lesseni watendaji waliokuwa wakihusika katika kitengo hicho wanamwambia aliyeenda kulipia kuwa mtandao aufanyi kazi acha pesa hapa utakapofanya kazi tutakukatia leseni, mfanyabiashara anatoa fedha hizo akirundi kesho yake maafisa hawa wanampa leseni yake lakini pesa aziwekwi kwenye mfumo bali kwenye mifuko yao ”
Sambamba na hilo,mkuu wa mkoa huo ametoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya wote mkoani humo pamoja na wakurugenzi wa halmashauri ndani ya halmashauri kuunda kamati ili wapitie vyanzo vyote vya mapato ndani ya wilaya zao na kuagiza kupatiwa majina ya wanya biashara wote kutoka wilaya zote na amekabidhi ripoti hiyo kwa TAKUKURU ili wote waliohusika katika vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ili uwe mfano kwa viongozi wengine wanaofanya vitendo kama hivyo.
“Unakuta mkaguzi amekaa miaka kumi ndani ya halmashauri lakini afanyi chochote akagui anaulizwa anasema hajawahi kukagua pale,tunatakiwa tuunge serikari yetu mkono katika ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri zetu ili mkoa wetu uweze kipiga hatua kimaendeleo, mkoa wa Kagera una fursa nyingi sana ziwa, ardhi pamoja na maeneo ya kufuga sasa mimi na wenzangu wakuu wa wilaya hatuta kubali mapato ya mkoa wetu yapotee”.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya halmashauri ya Bukoba Mheshimiwa Moses Machali amesema kuwa kamati teule ilifanya kazi ya kuchunguza ili kubaini upotefu wa fedha hizo ulianza tarehe 22/12/2021 na kutumia nafasi hiyo kuipongeza kamati ya uchunguzi pamoja mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba bwana Hamid Njovu kwa ushirikiano waliutoa ili kukamilisha uchunguzi huo.
“Naishukuru kamati uchunguzi kwa Kazi nzuri waliyoifanya lakini pia namshukuru mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba japo kuwa nimgeni lakini katusaidia sana,niseme kwamba uchunguzi huu ulichukua takribani wiki tatu hadi kukamilika na ulibaini wote waliohusika na ufujaji wa mamilioni haya ya fedha wanatoka katika kitengo cha mapato katika halmashauri yetu ya manispaa ya Bukoba na naamini ripoti hii iliyokabidhiwa kwa TAKUKURU itawasaidia kwani wamepata pakuanzia na sheria itachukua mkondo wake”
0 Comments