Header Ads Widget

WANAMUZIKI NYOTA WA KIMATAIFA KUTOKA ITALY NA URUSI KUTUMBUIZA KWENYE ZANZIBAR INTERNATIONAL FASHION WEEK 2021

 




NA MWANDISHI WETU.


Wanamuziki nyota wa Kimataifa kutoka Mataifa ya Itali na Urusi wanatarajiwa kutoa burudani kwenye tamasha kubwa la Kimataifa la Ubunifu wa mavazi lijulikanalo kama Zanzibar International Fashion Week kupitia mwavuli wa "Runway bay fashin week 2021".


Kwa mujibu wa Meneja wa  Tamasha hilo, Ahmed Harith amesema wanatarajia uwepo wa wanamuziki hao nyota wa Kimataifa ambapo kutoka Urusi  mwanamuziki Julia Makarova atato burudani na kutoka Taifa la Italia Mwanamziki, Laura Candy atatoa burudani.


"Wanamuzi hao watakuwa chachu na ni miongoni mwa wanamuziki nyota katika Mataifa yao.



Hii sio ya kukosa  bila ya kusahau Dj wa Kimataifa ni special fashion Dj worldwide kutoka Afrika Kusini ajulikanae kama Glo Susini" alisema Ahmed Harth.


Aidha, amebainisha kuwa, siku hiyo ya ufunguzi ya 26 Desemba, kutakuwa na 'parade' ambayo itamalizia ngome kongwe ambapo kutaendelea na fashion na music and art performance. 


"Kwa siku ya tarehe 27 Desemba kutakuwa tukio  kubwa la  fashion maeneo ya Forodhani  mizingani eneo la 'Sea front' ambapo tunafanya maonesho ya ubunifu kwa watu wote waone kutakuwa na waalikwa mbali mbali viongozi wa Serikali, ofisi za mabalozi , wafanyabiashara, wawekezaji, wasanii na wadau mbali mbali." Alisema Ahmed Harth.


Aliongeza kuwa "Tarehe 8 Marumaru hotel ni siku ya utoaji wa zawadi kwa wabunifu , Djs, Models na wale waliona mchango mkubwa katika sanaa ya ubunifu wa mavazi.


"Tarehe 29 Desemba  ni siku ya mbio za ngarawa (dhow race) na kufuatiwa na After party itakayofanyika katika ukumbi wa Cape town fish market.



Lakini pia katika wiki ya uwepo wa Zanzibar Fashion Week kutakuwa na  Panel discussion kuhusiana na Fashion, business na Tourism ambapo kutakuwa na waudhuriaji kutoka mataifa mbali mbali kwa siku ya tarehe 26 katika ukumbi wa Marumaru hotel." Alimalizia Ahmed Harth.


Katika hatua nyingine Meneja huyo amebainisha kuwa, Tarehe23 - 24 ni siku ya kufanya vipimo kwa models  wote katika ukumbi wa Marumaru hotel uliopo Unguja.


"Mazoezi ya models yanaendelea Marumaru hotel mpaka tarehe 21. Pia kutakuwa na maonesho ya wajasiriamali mbali mbali (women empower) maeneo ya Forodhani ambayo yataanza tarehe 23 - 29 December mwaka huu.


Ambapo pia kutakuwa na warsha ya upambaji kwa kutumia vipodozi, warsha ya watumiaji wa mitandao ya kijamii juu ya faida ya mitandao ya kijamii juu ya fashion ambayo yataendeshwa na mwandishi wa habari kutoka Urusi Ingrid Kim.


Pia kutakuwa na warsha ya masuala ya Haki miliki (intellectual property).


Mwaka huu linakuwa ni la msimu wa pili ambapo kusudio la tamasha hili ni kuweza kuwawezesha wabunifu wa mavazi kuuza kazi zao na pia kuleta wigo wa wawekezaji kuwawezesha wabunifu wa mavazi. 


"Kwa mwaka jana liliweza kuhudhuriwa na watu wasiopungua 3000 katika majukwaa matatu kwa siku tatu. 


Changamoto kubwa ya tamasha ni kukosa wafadhili,  Ingawa hilo haliturejeshi nyuma kwani tumeandaa mipango mikakati kwa kuweza kufanikisha kwa tamasha hili ambapo dhamira yake ni kuwa kutanisha wabunifu kutoka nchi mbali mbali kwa kuonesha tamaduni za nchi zao kupitia ubunifu wa mavazi." Alisema Ahmed Harth



Aidha alibainisha kuwa, Tamasha hilo linachangia kwa kiasi kikubwa kupitia uchumi wa nchi kwani wahudhuriaji wengi wanatoka nje ya nchi kwa kuwa watahitaji kukaa mahotelini , kula , kutembelea vivutio vya utalii.


"Wito wetu kwa Serikali na wadau wengine ni kushirikiana na kuunga mkono tamasha ili kuweza kutangaza nchi yetu kwa kupitia ubunifu .


Kwa kuwa lengo letu ni kudumisha na kutangaza tamaduni zetu." Alimalizia Ahmed Harthi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI