Header Ads Widget

VIONGOZI WATAKIWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Viongozi mbalimbali Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutatua kero za wananchi na kuepuka siasa za chuki miongoni mwao na badala yake wawe wamoja ili kuleta maendeleo. Mwandishi Rehema Abraham

 Mkuu wa wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro mh. Abas Kayanda ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi  mbalimbali katika mkutano  wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Ccm Jimbo la vunjo kwa kipindi Cha mwaka 2020/2021 uliofanyika Himo mkoani Kilimanjaro.

Aidha amesema wananchi wanachohitaji ni maendeleo hivyo ni amewataka  viongozi hao kujikita katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kutenda haki kwa wananchi.


Katika hatua nyingine amesema kuwa viongozi wengi ni wamoja na wametoka katika Chama kimoja lakini bado wanagombana kwa kugombania maslahi Yao binafsi jambo ambalo sio sahihi.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo hilo la vunjo Mh.dr.Charles Kimei amesema kuwa kumekuwepo na mafanikio yameweza kuonekana na Mwanga mpya imeonekana katika Jimbo Hilo.

Pia amesema kuwa katika maendeleo hakuna kata inayobaguliwa katika maswala ya maendeleo kwani kununua kata zingine zimeomba miradi Kama zahanati lakini hawana eneo la kujengwa zahanati hiyo .

Naye Katibu wa Ccm wilaya ya Moshi vijijini Ramadan Samweli   amemtaka Kila diwani bàada ya kikao hicho kuandaa taarifa ya ilani ya Chama Cha mapinduzi na kuwasilisha katika halmashauri kuu ya kata ili kurahisisha kupatikana kwa Mkuu wa wilaya.

Hata hivyo mkutano huo wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Ccm Jimbo la vunjo kwa kipindi Cha mwaka 2020-2021 umeandaliwa na mbunge huyo ambapo umewashirikiaha madiwani wa Jimbo hilo , wenyeviti wa kata,makatibu wa kata , makatibu wenezi wa kata.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS