Header Ads Widget

TGNP YAANDAA MJADALA JUU YA HALI HALISI YA UTEKELEZAJI WA (MTAKUWWA)

 



MKURUGENZI  Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Lilian Liundi amesema  asilimia 3.5 ya  fedha  za pato la Taifa zimekuwa zikipotea kutokana kushughulikia vitendo vya kikatili wanaofanyiwa wanawake na watoto wakike.


Akiongea leo Desemba 15,2021 katika Majadiliano  ya utekelezaji wa mjadala juu ya hali halisi ya  Mpango Kazi wa Taifa  Wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA ) Mkutano uliokutanisha wadau 

Mbalimbali ikiwemo wawakilishi wa asasi mbalimbali za kirai pamoja na Wabunge Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema ukatili unaghalama na kumekuwa ukirudisha maendeleo ya kifamilia nyuma na taifa kwa ujumla.


"Tumekuwa tukipoteza fedha nyingi katika mapambano haya ya ukatili na sisi kama mashirika ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto tunaendelea kupambana kwa kuhakikisha tunatokomeza vitendo vyote vya ukatili," amesema Mkurugenzi Lilian.


Na kuongeza kueleza kwamba "Mikakati ya MTAKUWWA imekuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na vitendo vya kikatili ambapo hadi sasa madawati ya jinsia yameanzishwa na kufikia 420 ," amesema .


Awali kifungua Majadiliano hayo Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto  Stuni  Msangi amesema  katika kuanzisha madawati ya jinsia jumla ya Wahanga 58,0059 wameripoti kufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali .


"Tuseme wazi taifa lisilo na ukatili wa kijinsia ni taifa lenye Maendeleo na niwazi kuwa usalama wa mwanamke na mtoto wa kike ni chanzo kikubwa cha Maendeleo katika nchi.


Aidha,Msangi amesema asilimia 40% ya wanawake wamefanyiwa ukatili katika kipindi cha maisha yao.


Nao Wadau wa mbalimbali wa kupambana na ukatili wakiwemo wambunge  wamesema zinahitajika nguvu za pamoja katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI