Header Ads Widget

TBA YAJIPANGA KUKARABATI MAJENGO KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI



Wakala wa Majengo Nchini (TBA) imesema imetumia shill milioni 515 kukarababi wa Majengo 60 katika Jiji la  Dar es Salaam, ambapo inatarajia kukarabati nyumba na majengo 6848, huku ikiwa jumla ya nyumba 45 zimeshakarabatiwa Jiji la Dodoma.......Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam



Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua Majengo 14, Kaimu Mkurugenzi Msimamizi wa Miliki Said Mndeme ambapo amesema wamejipanga kukarabati majengo yote yanayomilikiwa na TBA nchi nzima Ili kuzipa muonekano bora kabisa.


Aidha, amesema ukarabati huo umefanywa kwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya TBA  ambapo  umehusisha nyumba za viongozi, watumishi wa serikali, katika mpango wa awamu ya kwanza.



Amesema kuwa, hatua ya kukarabatiwa kwa Majengo hayo ni kutokana na dhana ya kuwa majengo ya Serikali yamechakaa sana, hivyo mpango wa kukarabati majengo hayo utafuta dhana hiyo.


"Kutokana na dhana hiyo ndiyo maana mwaka jana tumekuja na mpango maalumu  wa kuboresha makazi  nchini ambapo kwa Dar es Salaam jumla ya nyumba 60 zimekarabatiwa, ambapo ukarabati huo pia utaendana na kampeni ya usafi."amesema Mndeme.



Kwa upande wake,  Meneja Umiliki wa TBA, Fred Mangula ameishukuru Serikali kwa kuwapa sh.bilioni 23  katika mwaka wa fedha 2021/ 2022 kwa ajili ya kukarabati majengo hayo nchini.


"Mikakati ya TBA ni kujenga nyumba nyingine mpya kwani uhitaji ni mkubwa  na tayari tumeanza ujenzi wa nyumba 150 (Dodoma), Magomeni(20) na Masaki (10) kwa Dar es Salaam,"amesema Mangula.



Naye, Anne  Silayo mkazi wa Mbezi amesema jambo ambalo limefanywa na TBA ni zuri sana kwani nyumba hizo zimekua na muonekano wa tofauti, baada ya kufanyiwa ukarabati TBA.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI