Kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali katika uendelezaji wa tasnia ya mbegu kumekuwa na mafanikio makubwa kwenye uwekezaji wa mbegu ambapo Tanzania imeonysha kuwa ni nchi mojawapo yenye matumizi bora ya mbegu za kilimo......NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Hayo yalisemwa na Samson Poneja afisa kilimo mwandamizi idara ya maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo wakati akiongea na waandishi wa habarikatika mkutano TASAI wa kufanya tathimini ya mbegu kwa miaka mitatu ambapo alisema kuwa kilichofanyika ni kuhakikisha serikali inafanya kazi karibu na sekta binafsi ili kuwajengea mazingira mazuri ya kukua na kuongeza uzalishaji wa mbegu nchini.
“Uzalishaji wa mbegu umeongezeka kutokana na sekta binafsi kuwekeza kwa wingi tofauti na miaka ya nyuma ambapo tulikuwa tukiagiza mbegu nyingi kutoka nje lakini kwasasa sehemu kubwa ya mbegu tunazalisha ndani ya nchi,”Alisema Poneja .
Alifafanua kuwa lengo la serikali ni kuongeza uzalishaji wa mbegu hapa nchini ili ziweze kupatikana kwa gharama nafuu zaidi kwa wakulima lakini pia kuhakikisha wanatumia masoko wanayoyapata ya ndani na nje ya nchi vizuri kama vile soko walilolipata nchini China la maharage Soya ambayo kutokana na uzalishaji kuwa mdogo bado hawajaweza kujitosheleza katika soko hilo.
Alisema kuwa wanafanya kazi kwa karibu na balozi za Tanzania nchi za nje ambapo wanahamasisha watu watumie mbegu bora lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji na mwaka hadi mwaka wataalamu watafiti wamekuwa wakigundua mbegu za aina mbalimbali ambazo zinakuwa na sifa mbalimbali ikiwemo kuhimili mangonjwa na ukame na kuwa na uzalishaji mwingi.
Alisema kuwa mahitaji ya mbegu nchini ni takribani Tani 187000 lakini bado upatikanaji ni mbovu kwani mahitaji hayafikiwi lakini pia baadhi ya wakulima bado hawatumii mbegu bora na wanachokifanya ni kuwahamasisha na kuwaelimisha wakulima watambue umuhimu wakutumia mbegu bora.
Kwa upande wake Emmanuel Mwakatobe afisa kilimo mkuu kutoka taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu(TOSCI) alisema kuwa kwa sasa Tanzania imeonysha kuwa ni moja ya nchi inavyofanya vizuri kwenye matumizi ya mbegu bora za kilimo pomoja na udhibiti wa mbegu hizo ambapo mazao mengi ambayo wakulima wanayahitaji taasisi hiyo imekuwa ikiongeza udhibiti na kwasasa kuna upatikanaji wa mbegu nyingi.
“Mbegu ili iitwe mbegu bora ni lazima iwe safi na kukuidhi vigezo vyote vya afya ya mimea ambapo kama tukibaini mbegu ina magonjwa haitoruhusiwa kuwa chanzo cha mbegu bora na ndio mana tunawashauri wakulima wanunue mbegu ambazo tayari zimedhibitishwa na taasisi hii,”Alieza Mwakatobe.
Mshauri katika masuala ya kilimo Firmin Mizambwa ambaye pia ni mkurugenzi wa Agro inputs center alisema kuwa wamekutana kuwasilisha matokeo ya utafiti walioufanya katika makampuni ya mbegu ambao ulikuwa unaangalia sekta ya mbegu imekuwa kwa kiasi gani na wameeangali uzalishaji wa mbegu, sheria na masuala ya huduma kwa wakulima ambapo yote hayo wameyawasilisha ili kupata picha halisi ya maendeleo ya ukuaji wa sekta ya kilimo hapa nchini.
“Kwa maeneo yote tuliyoyapima tumeona sekta ya mbegu Imekuwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita ambapo kulikuwa na changamoto ya uwepo wa mbegu feki kwani mwaka 2016 tulipofanya utafiti kulikuwa na kesi 18 za uwepo wa mbegu feki lakini kwa mwaka huu imeshuka na kufikia kesi tano na huu ni mwendelezo mkubwa na maendelo,”Alisema.
Alisema wametoa mrejesho kwa wadau ili waweze kuona sekta ya kilimo na mbegu wamefikia wapi kwasababu matokeo hayo yanawasaidia kuweka mikakati kwaajili ya sekta hiyo na miaka mitatu ijayo waweze kukuta ukuaji wa kutosha katika sekta hiyo ambayo itakuwa ikitoa mbegu za kutosha kwa wananchi.
Naye Dkt Zubeda Omary mzalishaji wa mbegu kutoka mkoani Tanga alisema kuwa katika udhalisha wa mbegu bora kunahitajika utaalamu wa kipekee kwani ukishazipata mbegu ni lazima uzipeleke kwa wakulima na wazielewe ambapo tatizo kubwa lilipo katika usambazaji wa mbegu bora ni kuhitaji pesa nyingi hali inavyofanya gharama kuwa kubwa ambapo wakipata tasisi ambazo zinatoa taarifa kamaTASAI ambayo inawajusha mahali panapohitajika mbegu na kuna changamoto gani pamoja na kuweza kufika kwaajili ya utoaji wa Elimu.
0 Comments