Header Ads Widget

TARURA MWANZA WAJIPANGA KIVINGINE

 



Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura)Mkoa wa Mwanza imejipanga kumalizia tatizo la Ubovu wa Barabara zenye kero na zisizo pitika Kwa urahisi kutokana na Serikali ya awamu ya Sita kuona umuhimu Katika suala Hilo na kusikia kilio Cha Wananchi  kuwepo kwa Ubovu wa baadhi ya Barabara na nyingine kutopitika. ......Na Chausiku Said_Mwanza 


Mhandisi Godrack Mbanga ni Meneja wa Tarura Mkoa wa Mwanza ambaye alieleza kuwa, Mkoa unajumla ya Kilometa 8586 za Barabara zilizopo Katika halimashuri nane za Magu, Kwimba, Misungwi, Sengerema, Ilemela,Buchosa, Ukerewe na halimashuri ya Jiji la Mwanza(Nyamagana).



Mbanga anaeleza kuwa Awali Mkoa wa Mwanza ulishindwa kufikia Malengo yake Kutokana na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti waliyokua wakipewa Kutoka Serikalini kwaajili ya ukamilishaji na ujenzi wa Barabara Jambo ambalo lilisababisha baadhi ya Miradi kutokamilika Kwa wakati na mingine kutotekelezwa.



" Niipongeze Serikali ya Awamu ya Sita Kwa kuwajali Wananchi wake Kwa kuongeza fedha kwaajili ya ujenzi wa Barabara Katika Kila Jimbo Ili Kuondoa kero zilizopo kwenye  Barabara nyingi." alisema Mbanga.



Alisema Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iliona tatizo Hilo na kulifanyia Kazi ambapo iliweza kutoa ongezeko Shilingi Million 500 Kwa Kila Jimbo.



Alieleza kuwa utekelezaji wa fedha hiyo tayali umekwisha fanyika Kwa hatua mbalimbali na wakandarasi wapo Katika hatua za ukamilishaji ma Miradi iliyotekelezw Kwa fedha hizo tayari Kwa kuikabidhi.



"Baada ya kuona tatizo la Ubovu wa Barabara bado ni Kubwa Serikali yetu sikivu iliongeza fedha Kwa Awamu ya pili zilizotoka na tozo za mafuta ambapo ilitunga Sheria ya mafuta na kutoa ongezeko Kwa kuchaji Shilingi 100 Kwa Kila Rita Moja ya mafuta na kupata Jumla ya Shilingi Bilion 322 Kwa nchi nzima" alisema Mhandisi.



Alisema Katika fedha hiyo, Mkoa wa Mwanza ulipokea kiasi Cha Shingi Bilion 9 na Million 500 huku Kila Jimbo likipata Bilion 1 na tayali fedha hizo zilishaanza kufanya Kazi ambapo mpaka Sasa umeshafanyika Usanifu wa Barabara na wako hatua za mwisho za kusaini Mikataba kwaajili ya kuanza ujenzi.



Zaidi ya Miradi 20 ya ujenzi na ujarabati wa Barabara imekwisha sainiwa Mikataba tayali kwaajili ya kuanza utekelezaji wa Miradi hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI