Waziri wa mambo ya ndani George Simbachawene amesema kuwa teknolojia zinazogundulika katika vyuo mbalimbali ni vema zikaingizwa katika uzalishaji ili kuweza kutatua changamoto zinazohitajika kutatuliwa katika jamii kupitia gunduzi hizo.........NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Simbachawene aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la wanafunzi waliosoma chuo cha ufundi Arusha(ATC) ambapo alisema kuwa tasisi zinazohusisha na kuendeleza gunduzi hizo ni vema zikachukua na kupeleka katika jamii ili kutatua changamoto za kiteknolojia zilizopo lakini pia kuionesha jamii kwa miaka 60 ya Uhuru ni teknolojia zipi na gunduzi zilizofanyika.
"Kuna mambo makubwa yamefanywa na wasomi na nilitegemea zikishagundulika ziende katika uzalishaji na sokoni na kuweza kuongeza pato la taifa lakini pia kuwa suluhu ya ajira hapa nchini,”Alisema Simbachawene
Alifafanua kuwa vitu walivyovigindia wasomi vinanyima upatikanaji wa ajira kwasababu hawavipeleki katika uzalishaji jambo ambalo kwasasa wanatakiwa watoke huko na kwenda katika uhalisia wa vitu hivyo kwenda moja kwa moja kutatua changamoto katika jamii.
Sambamba na hayo pia waziri Simbachawene aliwataka watanzania kuelekea sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kila mmoja kuhakikisha anakagua gari kupitia gereji zilizo na ubora kama vile gereji ya chuo cha ufundi Arusha ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kutokea wakati wa kwenda mapumzikoni kutokana na magari kuwa na hitilafu kwasababu ya kupaki muda mrefu bila kutumika.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa chuo Cha ufundi Arusha Dkt Mussa Chacha alisema kuwa kongamano hilo ni la pili ambapo katika kongamano hilo wameonesha mpango walionao wa kujenga kliniki ya matibabu kwa ajili ya kupata mahali ambapo wanafunzi watafanyia mafunzo kwa vitendo lakini pia kutoa huduma za afya kwa wanafunzi wa chuo hicho,wafanyakazi ana familia zao pamoja na watu wanaoishi karibu na chuo hicho.
“Tulianza kutoa degree ya Medical Engineering na vijana wetu wanajifunza kutengeneza vifaa vya hosipitalini na kwa hili tumefanikiwa sana na vijana wamepata ajira katika hospitali mbalimbali na Sasa tunaona tujikite zaidi kwenye utengenezaji wa viungo bandia vya aina mbalimbali na hii itafanya tuisaidie nchi kwa kufanya watu wenye ulemavu wa viongo kupata viungo na kuendelea na shughuli ya kujenga uchumi wanchi,” Alisema Dkt Chacha.
0 Comments