Header Ads Widget

PROF. MKENDA AONYA WALIOPANDISHA BEI MBEGU YA ALIZETI.

 





Waziri wa kilimo Prof. Adolf Mkenda amewataka wauzaji wa mbegu waliochukua mbegu ya Alizeti kutoka kwa wakala  wa mbegu za kilimo kuacha kuuza mbegu hizo bei ya juu badala yake wauze bei elekezi isiyozidi 3500.......NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


 Wakati huo huo Bodi ya ushauri wa  wakala wa mbegu za kilimo (ASA) wameiomba serikali kuzuia uvamizi unaendelea katika mashamba ya uzalishaji wa mbegu nchini kwa uvamizi huo unahatarisha usalama wa mbegu na chakula kwa ujumla.


Profesa Mkenda alitoa onyo hilo wakati alipokuwa akizindua Bodi ya ushauri wa  wakala wa mbegu iliyoenda sambamba na kutembelea mashamba ya ASA mkoa wa Arusha ambapo aliwataka wauzaji wa mbegu kuacha kupandisha bei ya Alizeti ambapo wanauza hadi elfu 7000 kwa kilo huku bei halisi ikiwa ni 3500.



“kulikuwa Kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa mbegu ya alizeti lakini ASA wameweza kulitatua tatizo hilo na kwasasa mbegu ipo na wauzaji wanaochukua kutoka huku kwenda kuwauzia wakulima lakini wanauza bei ghali na hii huku wakiwa wamenunua bei ndogo nawaomba waache kwani lengo la serikali ni kuondoa changamoto ya uhaba wa mafuta ya alizeti iliyotokana na kukosekana kwa mbegu,” Alisema Profesa  Mkenda.



“Niwatake wananchi mtakapouziwa mbegu zaidai ya 3500 msinunue acheni nendeni ASA bado zipo lakini pia niwaombe ASA wazidi kufanya ubunifu mbegu izidi kupatikana na nimeona ASA wanachakarika na wanajitahidi kufanya kazi bidii na namesaidia kutuliza kelele za uhaba wa mbegu ya alizeti iliyopelekea mafuta kupanda bei kutokana na asilimia 55 ya mafuta kuagiza kutoka nje,Alisema Profesa.




Kwa upande wake  mtendaji mkuu wa wakala wa mbegu za kilimo (ASA) Dkt Sophia Kashenge alisema  wamefika wamepeleka tani 19495 za alizeti katika mikoa 19 na halmashauri 24 ambapo kila aliyeomba mbegu amepata  lakini pia ASA wanazalisha mbegu aina 42 na zote zinaenda kwa wananchi lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya mashamba ya kuzalisha mbegu kuvamiwa.


“Tunaiomba serikali iipe suala la uvamizi wa mashamba yetu kipaumbele kwani ardhi inapotea na mahitaji ya mbegu nchini yanakadiriwa kufika tani laki tatu kwa mwaka na ili uweze kuwa na tani hizo shamba linatakiwa kuwa na ukubwa wa hekta laki moja na nusu hadi laki mbili jambo ambalo uvamizi ukiendelea kutakuja kuwa na shida kubwa ya upatikanaji wa mbegu Hali itayoathiri usalama wa chakula,” Alisema Dkt Kashenge.




Alifafanua kuwa wakijumlisha maeneo yote ya uzalishaji bado hawajafikia hekta elfu thelathini na  wanahitaji kuwana maeneo makubwa kwasababu uzalishaji wa mbegu unahitaji eneo la utengano kati ya mbegu na mbegu ikiwa ni pamoja na kutenganisha mazao ya wananchi na mazao ya mbegu.


“Ili kuzalisha mbegu Kwa mfano ya alizeti inatakiwa utengano wa mbegu angalau kilometa moja na nusu kutoka kwenye shamba hadi kufikia shamba kingine lenye aina hiyohiyo ya alizeti na yakisogeleana huwezi kuzalisha mbegu  na hivyo hivyo kwenye mazao ya mahindi na mazao mengine kwahiyo ni changamoto kubwa ndio maana tumeiomba serikali angalau itusaidie maeneo ya uzalishaji yasivamiwe,”Alifafanua Dkt Kashenge.



Alifafanua kuwa waposema kuwe na usalama wa chakula cha kwanza lazima wawe na usalama wa mbegu na ili uwe na usalama wa mbegu ni lazima wawe na maeneo ya kuzalisha mbegu lakini miji inavyoongezeka,  maeneo bora ya uzalishaji yanavyojengwa maeneo ya uzalishaji wa chakula yanapungua.


Alieleza mashamba ya serikali mengi yalikuwa hayana hati na mangi hayakuweza kutumika vizuri kwasababu kipindi cha nyuma mahitaji ya mbegu yalikuwa kidogo lakini pia uwezeshwaji ulikuwa mdogo Hali iliyopelekea mashamba kuvamiwa kwa kiasi kikubwa lakini kwasasa mashamba hayo yanatumika kwaajili ya uzalishaji na wanakazana kuyatafutia hati.


“Yale yaliyovamiwa ndo tunaingia kwenye migogoro na lengo letu ni kupunguza migogoro kwa mfano shamba letu ambalo ni la pili kwa ukubwa la Msimba tayari tumepoteza hekari 1000 ambazo zimerudishwa kwa wananchi kwaajili ya chakula, mashamba na ujenzi na tuna shamba la Arusha ambalo tayari tumeshaligawa kwa kiasi kikubwa kwa wale waliokuwa wamevamia tukawaachia lakini sasa hivi kuna maombi ya njia kupita katikati ya shamba kwenda kwenye kiwanda Cha ngozi,” alisema 




Alieleza kuwa unapoweka njia katikati ya shamba tayari unatoa eneo kubwa ambalo litakuwa ni akiba ya barabara na unapoteza sifa la shamba kuzalisha mbegu kutokana na mwingiliano kwahiyo tunaomba kiwanda hicho kuendelea kutumia njia ya awali kwani japo kuwa ni ndefu ila inafika kwenye kiwanda.



Naye  wake mwenyekiti wa bodi Ashura Kihupe kuwa bado changamoto ni nyingi kwani katika mashamba ya mbegu bado kuna uvamizi wa mifugo na wizi wa mbegu kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya sekata ya mbegu.


Benson Minja msimamizi wa shamba la mbegu za mboga mboga la wakala huyo lililopo Tengeru alisema kuwa kwa msimu ulioisha wameweza kuzalisha mbegu za mboga aina mbalimbali Tani 7 na kwa mwaka 2021/2022 wanamalengo ya kuzalisha tani 22 kwa kulima hekta 43.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI