Header Ads Widget

PRF. KAMUZORA: HATUNA BUDI KUJIVUNIA MAMBO MBALIMBALI YA MAENDELEO TULIYOYAPATA TANGU TUPATE UHURU.

 





Hayo yamesemwa na katibu tawala wa mkoa wa Kagera prf. Faustine Kamuzora akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge katika kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru Tanganyika( TANZANIA) mkoa wa Kagera liliyofanyika katika uwanja wa uhuru  ulioko manispaa ya Bukoba  mkoani humo na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbambali wa serikali,taasisi binafsi pamoja na wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali zilizopo mkoani humo......Na, Titus Mwombeki-Kagera.



“Nipende kusema tunapoadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika(TANZANIA) na miaka 59 ya Jamhuri mkoa wetu wa kagera umepiga hatua nyingi za kimaendeleo katika sekta mbalimbali hasa katika afya, kilimo na ufugaji, uvuvi, ujenzi wa viwanda, elimu pamoja na ujenzi wa miundombinu ya hasa barabara”.


Aidha , ameviomba vyuo mbalimbali  nchini  kuja mkoani kagera na kufungua matawi yao kwani mkoa huo nisalama na una maeneo mengi yanayoweza kusaidia katika ujenzi wa  vyuo hivyo.



Ameongeza kuwa, katika kusherekea miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika walitangaza mashindano ya insha kwa wanafunzi washule zote zilizopo  mkoani kagera, washindi walitajwa majina yao baada ya kupitia insha zilizoandikwa na kuwabaini wahindi lakini awakuambiwa zawadi gani watapewa hivyo amekutumia siku hii kutaja zawadi kwa washindi hao.


 “Nipende kusema tulitaja majina ya wanafunzi walioshinda shindano la uandishi bora wa insha lililoshirikisha ngazi ya shule ya msingi pamoja na sekondari, leo washindi watakabidhiwa vyeti na hapo baadaye tutawaita washindi hawa mkoani kwakabidhi fedha tasrimu kama zawadi ambapo mshindi wa kwanza atapewa shilingi milioni moja, mshindi wa pili atapewa shilingi laki saba na mshindi watatu apewa shilingi laki tano”.


Amehitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kuendelea kuenzi tunu njema za taifa ambazo ni umoja amani na mshikamano. 



Kwa upande wake Irene Siliro mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Bujunangoma ambaye pia ni miongoni mwawashindi wa uandishi bora wa insha amesema kuwa,tangu nchi imepata uhuru mwaka 1961 sekta elimu imepiga hatua sana ukilinganisha na kipindi kile.


“ Ukiangalia kipindi kile nchi yetu ilipopata uhuru ilikuwa na watu wachache ambao wanajua kusoma na kuandika lakini mpaka sasa watu wengi kupitia mfumo  wa elimu ulionzishwa na mwasisi wa taifa letu mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa hasa  K.K.K yaani Kusoma, Kuandika na kuhesabu umesaidia sana watu kujua kusoma na kuandika, lakini sera ya  elimu bure pia limesaidia sekta ya elimu kupiga hatua kwani kupitia elimu imewasaidia kupunguza gharama za kupata elimu”


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI