Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya msingi Serengeti Iliyopo Ukonga Jijini Dar Es Salaam Bwana Bihimba Nassoro Mpaya Amefika kumpa pole Mjumbe wa Kamati ya shule ya msingi Serengeti Dr Chacha Chapakazi kwa kufiwa na Mama yake mzazi.
Akizungumza na Matukio Daima msibani kwa Dr. Chacha Bwana Bihimba amesema kuwa amestushwa sana na taarifa za Kifo cha Mama Chacha lakini ndo hivyo alipangalo Mungu mwanadamu hawezi kulipangua
"Kwakweli msiba huu ni pigo kubwa kwetu, maana huyu ni mama yetu sote na hakika pengo lake kwetu haliwezi kuzibika kamwe , na mimi kama Mwenyekiti wa kamati nimefika hapa kwa ajili ya kutoa rambirambi yetu, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe" Alimalizia Bwana Bihimba.
Msiba utasafirishwa kwenda tarime kwa ajili ya mazishi.
0 Comments