Kulingana na taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Kenya zinadai kuwa msichana huyo alienda kupata matibabu katika zahanati ya Kimtwa mnamo Septemba 2020 ambapo tukio hilo lilitokea.
Baada ya kugundulika msichana Huyo ni mjamzito wazazi pamoja na mamlaka zingine kumhoji alikiri kupata ujauzito huo kwa muuguzi Huyo Wa zahanati ambaye naye baada ya kupata taarifa za kufichuka kwa matendo yake aliamua kutoroka ili kujificha.
Taarifa zingine zidai kuwa muuguzi huyo alihamishiwa katika hospitali nyingine ya Kitini.
Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mary's Languni Yatta, kwa sasa amejifungua mtoto wa kiume.
Jeshi la Polisi nchini Kenya limekiri kumshikilia mtuhumiwa huyo katika kituo cha Polisi cha Yatta ambapo hii leo jumanne anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Credit; Citizentv.





0 Comments