Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ametekeleza ahadi yake ya kuchangia mifuko hamsini ya Saruji iliyokuwa inalenga kuunganisha nguvu na wananchi wa vijiji vya Mji mpya na Mvuleni vilivyoko kata ya Mabogini kwenye ujenzi wa zahanati itakayohudumia vijiji hivyo viwili.......Na Gift Mongi_Moshi
Prof Ndakidemi alikabidhi Saruji hiyo kwa mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wananchi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo kutoka kwa afisa mtendaji wa Kijiji hicho
Aliwashauri wananchi kushiriki kikamilifu kwenye kuchangia ujenzi wa Zahanati hiyo kwani ikikamilika itapunguza kero ya wanakijiji kwenda mbali kupata huduma za tiba.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Diwani Wa Kata ya Mabogini Dr Bibiana Masawe, wenyeviti wa vijiji vya Mvuleni na Mji Mpya pamoja na watumishi mbalimbali wa serekali na wakazi wa vijiji hivyo viwili.
Kwa niaba ya kata ya Mabogini na wananchi wa vijiji vya Mvuleni na Mji Mpya, Mheshimiwa Diwani alimshukuru mbunge kwa mchango wake wa mifuko 50 ya Saruji iliyokuwa na thamani ya shilingi laki saba na elfu hamsini (750,000).
Baaada ya kukabidhi Saruji, mbunge pia alitembelea eneo la ujenzi na kujionea ujenzi unaoendelea
0 Comments