Header Ads Widget

MAISHA YA WATANZANIA YAZIDI KURAHISISHWA KWA HUDUMA ZA KIDIGITALI KUTOKA TIGO

 Infinix Hot 11 Play na HOT 11 zimezinduliwa nchini Tanzania

• Wateja kupata hadi GB 78 za intaneti bila malipo kwa mwaka mzima.

Dar es Salaam. Tarehe 8 Desemba, 2021. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidigitali ya nchini, Tigo Tanzania, imeshirikiana na INFINIX Tanzania kuzindua INFINIX Hot 11 Play ambayo itauzwa kwa rejareja kwa 360,000Tshs na HOT 11 405000Tsh.

Ushirikiano kati ya INFINIX na Tigo huwapa wateja zaidi - huku simu mahiri ya kisasa ikija na intaneti ya 78GB kutoka TIGO bila malipo kwa mwaka mzima. Meneja biashara Tigo suleiman bushagama akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema, “Ushirikiano wetu na INFINIX ni jambo la kujivunia kwa sababu unaendana vyema na maono yetu ya kusambaza ulimwengu mpya wa kidijitali kwa wateja. Uzinduzi huu wa aina nyingine ya juu zaidi, simu mahiri ya bei nafuu, ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia manufaa ya maisha ya kisasa yaliyounganishwa kupitia huduma na bidhaa tunazotoa.”

"Washirika wetu wanaendelea kuamini chaneli zetu za usambazaji, mtandao mpana wa 4G, Tunalenga kuongeza kasi ya kupenya kwa simu mahiri nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, ambapo mteja atakayenunua simu hizi kutoka kwenye maduka ya TIGO NA INFINIX atapata  data ya kuperuzi  mitandaoni ya GB 78 BILA MALIPO kwa mwaka mzima.” Alisema Bushagama.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Umma wa Infinix, Bi Aisha Karupa alisema “Tulibuni HOT 11 play na HOT 11 tukizingatia uzoefu wa mtumiaji kwa kuipa simu betri yenye uwezo wa kudumu na Chaji mda mrefu ya 6000mAh yenye chipset ya G37 kwa ajili ya utendaji wa kiwango cha juu kwa wale wapenzi wa GAMES pamoja na 6.82 silky. KIOO laini chenye kiwango cha  FHD+ na 90Hz ambacho kitamwezesha mtumiaji kutazama picha na Video kwa ubora uleule."

"HOT 11 inakuja ikiwa na kamera ya 50MP ya lenzi tatu yenye kipenyo kikubwa zaidi cha F1.6, ikiiruhusu kupiga picha nzuri mahala popote , teknolojia ya Super Charge, zote HOT 11 na HOT 11 Play zina 128GB Rom. na 4GB Ram itakayoifanya simu kuwa na kasi na nyepesi lakini pia Storage iyo itamsaidia mtumiaji kuhifadhi kumbukumbu zake za muhimu , kwakweli hii tunaweza kuiita funga mwaka maana tumekuletea simu bora kabisa na kwa bei nafuu , Karibuni maduka ya TIGO NA INFINIX kujipatia Infinix Note 11 play na HOT 11”.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI