MWENYEKITI wa Umoja wa Mabenki Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki zakubali kuanza kutoa riba nafuu hususani sekta ya kilimo ilikuongeza uzalishaji wenye tija na kuinua kipato cha mkulima na taifa.
Nsekela amekiri katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleo kwa wananchi kupitia sekta ya kilimo kuwa kwa kipindi kilefu mkulima alikuwa akiathiriwa na riba kubwa hata hivyo amesema ubunifu wa serikali umeleta suluhu ya kushusha riba hizo.
“Mikopo ilikuwa ikipatikana kwa riba kubwa, lakini nisema ubunifu wa Naibu Waziri (Hussein Bashe) umetoa uhakika wa kutoa mikopo kwa riba nafuu zaidi,” amesema Nsekela.
Benki ya CRDB inakusudia kutumia zaidi ya Sh bilioni 460 kuwanufaisha wakulima ikiwa ni pamoja na mikopo na bima za mazao. Amesema katika kipindi cha miaka mitano, mpango wa benki hiyo ni kuwafikia wakulima milioni 1.2 ambapo mikopo itatolewa kwa riba isiyozidi asilimia 10. Nsekela amedai katika mikopo yote iliyotolewa na mabenki, benki ya CRDB imetoa asilimia 45 kwa wakulima zaidi ya 750,000 kote nchini.
Idadi hiyo inahusisha wakulima 12,000 wa korosho, wakulima 300,000 wa pamba, wakulima 375,000 wa tumbaku na wakulima 8,000 wa kahawa. Tunatoa mikopo ya mbolea, kuandaa mashamba, mbegu na elimu kwa mkilima mmoja mmoja kupita vikundi.
Nsekela amesema tatizo lililokuwepo awali ni mikopo chechefu hata hivyo utaratibu wa mikataba na wanunuzi imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa sintofahamu ya mikopo kutolipika.
“Gharama zinakuwa juu kwa kuwa hakuna uhakika wa soko. Kufungua mahusiano ya nchi yanaongeza chachu kwa mabeki kuweza kukopesha. Na sisi kama CRDB tunapeleka benki yetu Lubumbashi. Tutasaidia wakulima na wafanyabiashara. Unapokuwa na mahusiano mazuri unaondoa vizuizi vya kibiashara.
“Kwenye kukopesha mabenki tunaliangalia hili. Mahusiano ya nchi na nchi yanapo kuwa mazuri unaongeza confidence kwa mabenki na mwekezaji.”
Vilevile amesema benki yake inatoa mikopo ya kujenga viwanda kukuza thamani ya mazao ya kilimo.
0 Comments