ADELADIUS MAKWEGA-WUSM MBEYA
Azam Televisheni ya Dar es Salaam inatarajiwa kurusha moja kwa moja matangazo ya Kilele cha Tuzo za Filamu nchini kutokea Jijini Mbeya ambayo yataanza rasmi leo saa moja jioni na kumaliza saa sita ya usiku wa jumamosi ya Disemba 18, 2021 kutokea katika ukumbi Tughiimbe Jijini Mbeya.
Matangazo hayo yatarushwa moja kwa moja na Chaneli 103 ya Azam ya Sinema Zetu ambapo wasanii kadhaa wa filamu wanatarajiwa kulijongea jukwaa la tuzo hizo na marufaa kunyakua tuzo hizo na kutoa neno kwa Watanzania ambazo zimeandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Mandari ya eneo hilo zitakapotolewa tuzo sasa imepamba na basi kubwa la Azam la Matangazo ya Nje (Outside Broadcasting Bus) Higer T 331 DCM kuashirikia kuwa matangazo hayo yatakuwa mubashara.
Vifaa kadhaa vimeonekana vikiwa vimefungwa tayari kuanza kazi hiyo ya kuwapa burudani wa Kilele cha Tuzo za Filamu kutoka katika Jiji la Mbeya ambapo wasanii kadhaa wa muziki wataimba.
Akizungmzia namna watakavyorusha matangazo hayo, Nixoson Kabumbire ambaye ndiye msimamizi wa matangazo hayo amesema kuwa kwa upande wao wameshakamilisha kila kitu na hawatoweza kuiangusha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hilo.
“Matangazo yetu mara zote hayana chenga wala mikwaruzo ni nina wahakikishia Watanzania wezangu wataona kinachoendelea moja kwa moja kukiwa na ubora wa viwango vyote vya juu ambapo Azam pekee tutakuwa mubashara.” Alijigamba msimamizi huyo wa matangzo hayo ya leo.





0 Comments