Header Ads Widget

WATANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII, LHRC,TAS NA THRDC WALAANI MAUWAJI YA ALBINO

Watanzania  wametakiwa kuacha mila potofu za kuuwa watu wenye Ualibino kwa lengo la kujipatia utajiri badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waweze kupata kipato cha halali. mwandishi wa matukio daima Fatma Ally anaripoti kutokea Dar Es Salaam

Kauli hiyo aliitoa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  Anna Henga wakati akitoa tamko la  kulaani vikali  ufukuaji wa kaburi la marehemu Heri Kijangwa  ambae alifariki July 4, 2020 kwa maradhi ya Kansa ya ngozi.

Alisema kuwa, hakuna kiungo chochote cha binadamu ambacho kinaweza kumfanya mtu awe tajiri hivyo, jamii inapaswa kuondokana fikra potofu.

"Kwa Karne hii kweli mtu utajirike kwa kupitia viungo vya ualibino, nawaomba watanzania tuache mila potofu na badala yake tufanye kazi kwa bidii lakini sio kutegemea kumuua binadamu mwenzako, maana wameanza na alibino, kesho watu wafupi, mara wanene tutafika kweli"Alisema Henga.

Alisema marehemu Kijangwa ambae alikua mkazi wa kijiji Cha Tanda Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga mwili wake ulifukuliwa kaburini Oct 24 mwaka huu na watu wasiojulikana ambapo walinyofoa mguu wake wa kulia na kuelekea kusiko julikana.

Henga alisema tukio kama hili ni la pili kuripotiwa kati ya mei 3 na 4 mwaka huu ambapo mwili wa mtoto mwenye  ualibino aliyekua na umri wa takriban miaka 5 uliokotwa ukiwa umekatwa mikono yote miwili huko kijiji Cha Nondo , Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora na taarifa ya uchunguzi haijawahi kutolewa na jeshi la Polisi.

Aidha, alisema kufuatia tukio hilo kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC)  kwa kushirikiana  na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) pamoja na chama Cha watu wenye ualibino Tanzania (TAS)  wamelaani vikali vitendo hivyo vya kikatili na vya kinyama vinavyotweza utu wa Binadamu na vya kudhalilisha maiti.

"Kitendo cha kufukua mwili wa marehemu Heri ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu Cha 127 na 128 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019"alisema Henga. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TAS Mussa Kabimba alisema matukio ya mauaji kwa watu wenye ualibino yalikua yamepungua kwa miaka minne iliyopita lakini kwa sasa ndani ya miezi minne na nusu yameripotiwa matukio mawili hii sio taarifa nzuri.

Hata hivyo, alisema Serikali inatakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kupingana na vitendo hivyo sio tu pale linapotokea jambo, wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Naye, Afisa programu Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Perpetua Senkoro alisema kuwa, Ili kukomesha vitendo hivyo ni lazima wahusika wakuu wanaowatuma watu kufukua makaburi ama kufanya vitendo vya mauwaji  wakamatwe na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Aidha alisema matukio hayo ya mauaji awali yalikua yakifanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini kwa sasa yameenea kwenye mikoa yote, bila kuchukuliwa hatua kwa wahusika, matukio haya hayawezi kupungua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI