Wanahabari wamiliki wa mitandao ya kijamii wakiwa Katika mafunzo ya uboreshaji wa uandisha wa Habari unaozingatia ukweli
WITO umetolewa kwa wanahabari wa mitandaoni nchini Tanzania kuandika habari zenye ubora na weledi ikiwa ni pamoja na kutumia Takwimu za uhakika katika kuandaa habari huku badala ya kuandika vichwa vya habari visivyo na uhalisia ili kuvutia wafuatiliaji wa mitandao hiyo ya kijamii.
Wito huo umetolewa leo ( Novemba 01, 2021 )jijini Dar es salaam na mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen katika mafunzo ya Uhakiki wa Habari yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Tanzania (Tanzania Media Foundation TMF).
Dausen alisema kwa sasa Waandishi wengi wa Mitandao wanaandika Habari zisizo na vigezo vya Habari huku wakiacha masuala mengi muhimu ikiwemo takwimu, mizani na ukweli.
Alisema kuwa changamoto kubwa inayosababisha hali hiyo ni baadhi ya wamiliki wa Vyombo vya Habari mitandaoni kujali idadi ya watu wanaotembelea mitandao yao bila kuangalia kama habari walizoweka zinasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Dausen alisema kuwa kwa sasa wasomaji wa mitandaoni wameanza kuzikwepa taarifa zenye vichwa vya habari vya kuvutia ambavyo haviendani na uhalisia wa habari zenyewe.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Dastan Kamanzi alisema Waandishi wa Habari wanatakiwa kuwa na msingi wa awali, jumla na wa kubobea katika uandikaji wa habari.
Alisema kuwa msingi wa uandishi wa Habari ni ukweli hivyo ni muhimu Waandishi wa Habari kuzingatia msingi huo kila wanapoandaa habari zao.
Huku baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, Joseph Mwaisango pamoja na Asha Shaban wamekiri kwamba yatawasaidia kuboresha uandishi wao wa habari hususani kutumia takwimu na kuhakiki habari kabla ya kuchapishwa mtandaoni.
Mafunzo hayo ya Uhakiki wa Habari yamewajumuisha Waandishi wa Habari za mtandaoni kutoka mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mara, Mbeya na Iringa.
Hivi sasa mitandao ya kijamii nchini Tanzania imekuwa ni sehemu ya haraka kwa watanzania kupata habari mbali mbali na kupitia mafunzo hayo ni wazi wanahabari hao watasaidia kuongeza imani kwa wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii kuendelea kujenga imani na kupata habari za uhakika.
Matumizi ya mitandao ya kijamii ni mojawapo ya shughuli maarufu zaidi duniani. Mwaka 2018 pekee watu bilioni 2.65 walikadiriwa kuwa watumiaji wa mitandao kote duniani
Hata hivyo idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka na kufikia bilioni 3.1 mwaka 2021.
Watumiaji nao wamekua wakiongezeka ambapo Januari peke yake mwaka 2019 waliongezeka kwa asilimia 45.
Nchini Tanzania mtandao wa Instagram umekua maarufu sana na wenye watumiaji wengi, kwa matumizi ya burudani na biashara.
Mkurugenzi mtendaji wa Nukta Africa Nuzulack Dausen akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya uhakiki wa taarifa kwa waandishi wa habari za mtandaoni yanayofanyika jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Dastan Kamanzi akifungua mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Wanahabari wa mitandaoni wakiwa katika mafunzo ya siku tano yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanahabari wa mitandaoni wakiwa katika mafunzo
Picha na Habari Mussa Said, TMF, Francis Godwin (matukio Daima , William Bundala, Kijukuu Online ,George Binagi, BMG na mitandao ya kijamii
0 Comments