RPC wa Mwanza Ramadhani Ng'anzi
Watu watano wa familia moja mkoani Mwanza wamefariki dunia baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuwaka moto.MWANDISHI WA MATUKIO DAIMA MEDIA,CHAUSIKU SAID ANARIPOTI
Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi Ramadhani Ng'anzi amesema kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 6 usiku na kusababisha vifo vya watu hao.
Ramadhani amewataja kwa majina watu hao waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Lameck Denedictor umri (32) msukuma mkazi wa igoma, Leah Lameck umri (26) mkulima, Yunith Lameck umri (01) na vijana wawili wa kiume ambao majina yao hayajatambuliwa walioenda kutembelea nyumbani kwa marehemu.
Ameeleza kuwa chanzo cha moto huo uliosababisha maafa hayo makubwa bado haujajulikana na jeshi la polisi kwa kushirikiana na kikosi cha zima moto na uokoaji bado wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini tatizo lililopekekea vifo hivyo.
" bado tunafanya jitihada za uchunguzi ili kujua chanzo cha moto huo na kusababisha vifo vya watu wote hao wa familia moja'' alisema Ng'anzi
Ramadhani ameeleza kuwa thamani ya mali zilizoteketea katika nyumba hiyo bado haijajulikana mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.
Hata hivyo ameeleza kuwa miili ya marehemu imeifadhiwa katika hospital ya sekou- toure ili kusubiri uchunguzi wa madaktari utakapokamilika miili hiyo itakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
0 Comments