Header Ads Widget

MAAJABU YA KAKAKUONA HUYU.




WAKAZI wa eneo la Mpiji kata ya Maili Moja wilayani Kibaha walifurika kwenye eneo la mzee maarufu Mkwenya kumshuhudia mnyama adimu Kakakuona wakitamani atabiri lakini licha ya kiu yao hiyo hakuweza kutabiri chochote.


Balozi wa eneo hilo John Kimario alisema kuwa mnyama huyo alionekana majira ya saa 3 usiku Novemba Mosi.



Kimario alisema kuwa walimchukua na kumhifadhi kwenye nyumba ambayo haijakamilika na kumfungia ili aisije akatoweka kwa lengo la kuwakabidhi kwa idara ya maliasili.


Mzee Amiri Mkwenya (87) alisema kuwa kama kuna mtu mbaya kwenye eneo hilo hawezi kuonyesha ishara yoyote zaidi ya kujificha tu licha ya mara mbili kutaka kuamka lakini alipoona umati aliendelea kujificha.



Kwa upande wake ofisa maliasili wa Mkoa wa Pwani Felix Shayo alisema kuwa mnyama huyo ni miongoni mwa wanayama ambao wako kwenye hatari ya kutoka na ndiyo sababu wanapoonekana humchukua na kumrudisha msituni ili akaendelee na maisha yake.


Shayo alisema kuwa mnyama huyo huwa anaondoka kwenye makazi yake baada ya kuharibiwa na watu wamekuwa na imani kuwa wana uwezo wa kutabiri masuala mbalimbali jambo ambalo huawaachia walifanye kisha kumrudisha.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI