Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani alitoa Kauli hiyo jana wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) .
Alisema Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wanatakiwa wapate elimu na mbinu bora za ufugaji wa kuku ikiwemo namna ya kuwapa chanjo kwa ajili ya kuwakinga na magonjwa yanayowakabili na kuwafundisha juu ya ufugaji wa nyuki kupitia mizinga ya kisasa.
Balozi Dkt. Batilda alisema maeneo mengine ambayo wanapaswa kupewa elimu ni kuhusu uendeshaji wa biashara na uundaji wa vikundi kwa ajili ya uzalishaji mali.
Alisema hatua hiyo itawasaidia kufanyakazi kwa juhudi na kujiletea maendeleo, hali itakayowafanya kuacha kutegemea fedha za TASAF na hivyo kutoa fursa kwa wahitaji wengine kupata fedha hizo.
“Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan anapenda wananchi wake waendelee, na maisha ya Watanzania yabadilike watoke walipo na kusonga mbele na kupata maendeleo ya kweli” alisema.
Aliwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii hao kwenda kuwafundisha jinsi ya kuibua miradi ambayo itawasaidia wenyewe.Katika hatua nyingine wakazi wa Ifucha walimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuwafikishia kilio chao cha bei ya Mbolea kupanda juu ambapo itawafanya washindwe kulima.
Chiku Rashid alisema bei imepanda sana kutoka elfu 60 hadi laki moja jambo ambalo linaonekana ni mzigo kwao.
Said Haruna alisema kuwa udongo wa Tabora ni mchanga bila matumizi ya mbolea hakuna mavuno.
Balozi Dkt. Batilda alisema kilio chao atakifikisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
0 Comments