Header Ads Widget

MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA WANANCHI WAPATA MAFANIKIO MAKUBWA.

 


Na Hamida Ramadhani Dodoma 


KATIKA kusherekea Miaka 60 tangu nchi ipate uhuru mafanikio makubwa yameonekana ndani ya taifa la Tanzania kwa kuongezeka kwa ajira katika utumishi wa umma kutoka watumishi 17,566 mwaka 1961 hadi 528,290 mwezi Ocktoba, 2021 kati ya hao watumishi wa sekta afya wamefikia 72,961sawa na asilimia 13.8 na walimu wamefikia 281,729 sawa na asilimia 53.3.


Akiongea leo na waandishi wa habari jijini hapa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa amesema katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru utumishi wa umma umeendelea kuwa uliotukuka katika kuchangia ustawi wa Taifa.


"Hatuwezi kutambua na kuthasimini hatua kubwa tuliopiga kama taifa katika kujijengea uwezo wetu wa kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuendeleza taaluma mbalimbali ndani ya miaka 60 bila kujua tulikotoka,"amesema 


Na kuongeza kusema"Wengi wetu hatujui Tanganyika ilipopata uhuru tulikuwa na madaktari 12 tu nchi nzima na wahandisi wawili huku asilimia 58 wananchi walikuwa hawajui kusoma wala kuandika ni ukweli kwamba hatujafika tunakotaka kufikalakini tumepiga hatua kubwa kwwnye nyanja zote za kujenga nguvu kazi,"Amesema Mchengerwa. 


Akiongelea suala la vyeti feki Waziri Mchengerwa jumla ya watumishi 4195 waliondolewa kwa kugushi veti vya kidato cha 4 wamerudishwa kazini baada ya kujiendeleza na kupata vyeti ambapo kati yao watumishi 1150 walioshindwa kujiendeleza wametakiwa kulipwa stahiki zao kutokana na utenadji kazi wao wa kazi uliotukuka.


Mwishoo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI