Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Kamol amempongeza Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo Shule za Sekondari nchi nzima. mwandishi Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akihitimisha ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Jimbo hilo, ambapo lina shule za Sekondari 17, katika Kata 13 ambapo walikua na upungufu wa vyumba vya madarasa 125 .
"Upungufu huu ulisababisha baadhi ya shule zetu kuwa na awamu mbili za wanafunzi kuhudhuria masomo yao (double shift) jambo ambalo lilisababisha kutokuleta ufanisi wa kazi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi" amesema Bonah.
Amesema kuwa, Rais Samia amelipatia jimbo hilo jumla ya shill bill 1,72000,000 Ili kujenga vyumba vya maradasa 86 ambavyo vimepunguza upungufu wa vyumba vya madarasa kwa asilimia 68.8, ambapo watakua na upungufu wa vyumba vya madarasa 39 sawa na asilimia 31.2.
Aidha amesema kuwa, jumla ya shule zilizopata mgawanyo wa fedha hizo ni 11 ikiwemo Shule ya Sekondari Zawadi iliyopo Kata ya Tabata ambapo imepewa shill mill 240 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa, Bonyokwa imepewa shill mill 240 kwa ajili madarasa 12.
Ameongeza kuwa, shule nyengine ni Shule ya Sekondari kiwalani iliyopo Kata ya Kiwalani imepwa shill mill 240 kwa madarasa 12, Minazi Mirefu iliyopo kata ya kipawa imepewa shill mill 160 kwa madarasa 8 pamoja na Majani ya Chai iliyopo Kata ya Kipawa ambayo imepewa shill mill 40 kwa madarasa 2.
Pia amesema, shule nyengine ni Kisungu iliyopo Kata ya Kinyerezi imepewa shill mill 160 kwa madarasa 8, Kimanga Sekondari shill mill 80 kwa madarasa 4, pamoja na Magoza iliyopo Kata ya Kisukuru shill mill 100, kwa madarasa 5 .
Hata hivyo, amesema shule nyengine ni Kinyerezi iliyopo Kata ya Kinyerezi imepewa shill mill 160 kwa madarasa 8, Kinyerezi mpya ipo kata ya Kinyerezi shill mill 60 kwa madarasa 3, Buguruni Moto ilioyopo Kata ya Buguruni shill mill 240 kwa madarasa 12.
Hata hivyo, amesema watahakikisha wanashirikiana na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam na viongozi wengine wote kuanzia ngazi ya mitaa pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia kwa kuwajengea vyumba vya madarasa Ili kuweza kuondokana kabisa na upungufu wa vyumba vya madarasa katika jimbo hilo.
"Baada ya kumalizika ujenzi wa vyumba hivi vya madarasa, hatutakua na double shift tena katika shule zetu na wala hatutakua na mlundikano wa wanafunzi wengi katika darasa moja, jambo alilolifanya Rais Samia ni kubwa sana kwa wanasegerea na watanzania kwa ujumla"amesema Bonah
Amesema kuwa, wametembelea katika shule zot ujenzi unakoendelea wamejionea hali halisi ya ujenzi unavyoendelea, watanzania wanatakiwa kuungana kwa pamoja Kumshukuru Rais Samia na kumuombea kwa MwenyeziMungu Ili aendelee azidi kuleta maendeleo.
0 Comments