Header Ads Widget

DKT. GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA RED CROSS.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe kutoka Shirika la msalaba mwekundu (Red Cross) ulioongozwa na Rais wa shirika hilo David Mwakiposa Kihenzile na Mkurugenzi wa Afya Shirika hilo Dkt. Hilary Ngude. mwandishi wa matukio daima Andrew Chale anaripoti kutokea Dodoma

Katika Mkutano huo Wajumbe wa Shirika hilo walipata nafasi ya kuelezea historia fupi ya kuanzishwa kwa Shirika hilo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sheria namba 71 ya mwaka 1962 pamoja na marekebisho yake namba 4 ya mwaka 2019, majukumu yake, changamoto na malengo waliojiwekea katika kuelekea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Tanzania. 

Aidha, kwa pamoja walikubaliana kushirikiana katika kulisaidia Shirika hilo kukua ili kuisaidia Serikali kuwahudumia wananchi kwa ubora unaotakiwa. 

Aidha, Dkt. Gwajima alimhakikishia utayari wa Wizara yake kushirikiana na Shirika hilo la Msalaba mwekundu (Red Cross) katika kuboresha utoaji huduma kwa Watanzania na kuleta matokeo chanya katika Sekta ya Afya nchini. 

Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ya Waziri wa Afya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI