Viongozi wa ngazi mbalimbali Chama Cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi mjini na Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro wamepewa elimu ya jinsi ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na kuhakikisha kuwa mifuko ya uchaguzi unandaliwa mapema na muongozo pamoja na nyaraka mbalimbali ambazo zitatumika wakati wa uchaguzi ujao. mwandishi wa matukio daima Rehema Abraham anaripoti kutokea Kilimanjaro.
Akiwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo kwa viongozi hao Solomon Itunda Katibu msaidizi Mkuu idara ya oganaization Ccm Taifa , alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha zoezi la usajili wa Chama Cha mapinduzi (CCM) na jumuiya zake ziweze kutumia mfumo wa kielektronick.
Aidha alisema kuwa viongozi walioshiriki katika mafunzo hayo ni pamoja na viongozi wa kata ,makatibu wenezi wa kata,wenyeviti wa mashina ,madiwani wa ccm wa kata ,madiwani viti maalum,wabunge pamoja na secretaretariet ya wilaya na kamati ya siasa ya halmashauri ya Chama Cha mapinduzi.
"Kama mnavyoelewa dunia ya Sasa hivi imekuwa Kama kiganja ,Kuna mabadiliko makubwa sana ya Tehama na sisi Kama Chama Cha mapinduzi ambacho kimeshika Dola kwa Muda mrefu sana ndani ya nchi yetu hatuko tayari kuachwa nyuma timeanza zoezi hili mwaka 2008 na tunaendelea nalo ,kuhakikisha kwamba wanachama wetu wote kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa wanasajiliwa kwa mfumo wa kielektronick"Alisema Itunda.
Katika hatua hatua nyingine alisema kuwa kwa mujibu wa misingi ya Chama kinaendeshwa na taratibu ,kanuni na miongozo mbalimbali kwani inapofikia kipindi hiki Cha uchaguzi wanakuwa na jukumu la kuwambushana viongozi Mambo ambayo yanayopaswa Kupewa kipaumbele wakati wa kipindi Cha kuelekea uchaguzi.
Hata hivyo aliwataka viongozi hao kuanzia kufanya mapema maandalizi ya uchaguzi ,pamoja na kutenda haki katika mchujo pale wanapochagua viongozi katika ngazi mbalimbali .
Kwa upande wake Hashim Iddy mandari mjumbe wa halmashauri kuu Ccm wilaya ya Moshi vijijini amesema mafunzo hayo yamekuwa wakati muafaka kwani wapo kwenye kipindi Cha uchaguzi wa Serikali za mitaa.
"Mafunzo hayo ni muhimu wakati huu kwani yanafungua viongozi,na wanaelewa ,lakini pia mtoa nada amegusa zile sehemu muhimu Kama mtafaruku wakati wa uchaguzi,kwani wanaelewa Kila kitu ,hivyo wakati wa uchaguzi unapokaribia wanakuja kutuelimisha ili kuondoa tofauti zetu ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati wa kugombea nafasi za uongozi"Alisema Iddy.
0 Comments