Header Ads Widget

BITEKO; KAMPUNI ZA UCHIMBAJI MADINI CHANGIENI HUDUMA ZA MAENDELEO KWA JAMII

WAZIRI Dotto Biteko amezitaka Kampuni zote zinazochimba na kuchakata madini ya ujenzi ya kokoto kuhakikisha wanaandaa mpango wa kuchangia huduma za maendeleo kwa jamii inayowazunguka kulingana na vipaumbele vya eneo husika. mwandishi wa matukio daima John Gagarini anaripoti kutokea Pwani

Biteko aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kerai Construction, Even Enterprises, Gulf concrete pamoja na Saint Maria inayojishughulisha na  uchimbajii wa madini ya ujenzi ya kokoto iliyopo katika eneo la Lugoba wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema kuchangia huhuma za maendeleo kwenye maeneo yanayozunguka migodi si jambo la hiyari bali ni takwa la kisheria hivyo makampuni yakae na Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya ili mjue vipaumbele vya wilaya katika kuchangia huduma za maendeleo kwa jamii inayowazunguka.

Aidha aliyataka makampuni yenye migodi inayojishughulisha na uchimbaji wa kokoto katika eneo la Lugoba lazima iandae mpango wa ufungaji wa mgodi baada ya kumaliza uchimbaji na yawasilishe Tume ya Madini kwa ajili ya kusimamia utekelezaji.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wamilki wa migodi ya kuchimba na kuchakata madini ya ujenzi ya kakoto kufuata taratibu na Sheria zilizowekwa na Serikali.

Alizitaka kampuni hizo kulipa maduhuli ya serikali kwa kutumia mfumo wa POS ili kupata taarifa sahihi za mauzo na kudhibiti udanganyifu kwenye makusanyo ya mapato ya serikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI