Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Rais Mstaafu mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amefurahishwa na idadi ya wanafunzi wa kike kuongezeka mwaka hadi mwaka katika chuo hicho .
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akiwatunuku vyeti wahitimu 4121 wa awamu ya pili katika ngazi ya digrii ambapo ameutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha wanafikia usawa wa kijinsia kwa asilimia 50 kwa 50.
"Nimesikiliza hotuba yako Makamu Mkuu wa chuo nimefurahishwa na takwimu kwamba wahitimu wote wapo 4121 lakini kati ya wanaume ni 2101 na wanawake i 1920, hatua hii ni nzuri sana, usawa wa kijinsia kwa wahitimu wa shahada za awali unaonekana kupanda hivyo nawapongeza sana kwa hatua hiyo," amesema Dkt. Kikwete.
Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dr. William Anangisye amewataka wahitimu hao kuwajibika kwa kutumia elimu zao kuwa na ushawishi wa kuleta chachu ya maendeleo katika Taifa na Dunia kwa ujumla, kufanya kazi kwa bidii.
"Naomba mukaendelee kukipa heshima chuo chetu musiende kufanya mambo yoyote ya kukishusha hadhi, msiende kutegemea kuajiriwa Serikalini,bali mkawe chachu yakutengeneza ajira, mfanye kazi kwa bidii, muwe na nidhamu kazini"amesema Prof Anangisye.
Aidha, amesema jumla ya wahitimu 4121 wanahitimu katika ngazi ya cheti Shahada na Astashahada katika mahafali ya 51 ya Chuo kikuu cha Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jiijini Dar es salaam.
Naye, Mwayekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM), Jaji Mstaafu Damian Lubuva ameshukuru hatua zinazochukuliwa na Rais Samia za kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19, huku akiwataka wanafunzi na wahitimu hao kuendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo ili kumuunga mkono Rais Samia.
0 Comments