Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA WA VIFAA VYA UJENZI DODOMA WAONYWA.



 Na Hamida Ramadhan Dodoma 


WAFANYABIASHARA wa vifaa vya ujenzi mkoani Dodoma wametakiwa kuacha kupandisha bei za bidhaa zao badala yake wametakiwa kuuza kwa kizingatia bei elekezi ya serikali.


Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kupokea fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la fedha Duniani (IMF) kwajii ya kupambana na ugonjwa wa Corona ambapo mkoa wa Dodoma umepokea jumla ya shilingi Bilioni 17.97 kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo


Akizungumza leo na wafanyabishara hao Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema fedha hizo ni fursa kubwa kiuchumi kupitia Biashara  kwani fedha hizo zinakwenda kwa wafanyabiashara wazalendo wakati na wadogo ili kuwainua.



Amesisitiza fedha hizo zimetolewa lengo ni kwenda kuwanufaisha sekta binafsi na wafanyabiashara wadogo na wakati hivyo ni marufuku bidhaa za ujezi kupandishwa bei kiholela .


" Naendapo ikatokea au kujulikana nyinyi wafanyabishara mmepandisha bei kiholela serikali ya mkoa itakwenda kununua bidhaa na vifaa vya ujenzi mikoa mingine," amesema Mtaka


Pia amesema kupitia fedha hizo sekta binafsi inakwenda kukua na hata uchumi wa mtu mmoja mmoja kwani kupitia fedha hizo kila kata imepitiwa na ujenzi wa miradi ya kimaendeleo .


" Sasa niwaombe wafanyabiashara  fedha zimetufikia sasa tusilale tuchangamke soko hilo masuala ya kulala unafungua duka saa sita mchana  msije kumtafuta mchawi ," amesema mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka. 


Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo amesema fedha hizo ni fursa kubwa kwenye uchumi kupitia biashara kwani fedha hizo zinakwenda kwa wafanyabiashara wazalendo wazalendo wakati na wadogo.



"Nataka mtambue kwamba fursa zinazokuja lengo tunataka kuzalisha wafanyabishara mamilionea na mabilionea kupitia fedha hizi tunataka wafanyabishara wadogo wakue kikubwa tubadilishe bishara zetu,"amesema..


Sambaba na hilo waziri huyo amesema amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia mambo makuu matatu amabayo kutosheleza mahitaji kama ni kukupa mikopo waende kukopa fedha kwenye taasisi za kifedha kwani soko lipo la kutosha na waache imani za kishirikina .


Suala la pili ni kuzingatia Ubora Waziri huyo amesema kumekuwepo na shida  panapokuwa na mahitaji makubwa wafanyabishara wamekuwa wakichukua bidhaa bila kuzingatia ubora sasa kipindi hiki tutafuatilia ubora .


Na jambo la tatu ni kuzingatia maadili ambapo amewataka wafanyabiashara hao kusimama imara kwa kuuza bidhaa na kutoa listi tena ya mashine ya Efds.


Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Dkt Fatuma Maganga amewataka wafanyabiashara hao kuweka bidhaa zenye ubora na wazinagatie mahitaji na matakwa ya jiji linavyotaka kwani kila halmashauri inalangizake kwenye uezekaji wa mabati.


Naye mfayabishara Abdullah Taratibu Mratibu wa vijana wafanyabisharamkoa wa Dodoma TCCAI ameuomba uongozi wa mkoa tuoa ruhusa siku za Jumamosi  wafanyabiashara wote wafungue matuka yao mapema .


" Nikweli fursa ya fedha katikamkoa watu zimetufikia lakini nasisi wafanyabishara  biashara tunabanwa kufanya biashara siku ya Jumamosi kutakiwa lifungua maduka saa 4 wakati siku ya Jumamosi  ndio siku kubwa ya biashara,"amesema  kiongozi huyo.


Mwishoo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI