Header Ads Widget

THRDC WALAANI MAUJI YA KINYAMA KWA MTENDAJI WA MBEZI MSUMI




Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa pole kwa wakazi wa Mtaa wa Mbezi Msumi,familia,na Serikali,kufuatia kifo cha aliyekuwa Mtendaji wa Serikali wa eneo hilo,Kelvin Mowo,aliyevamiwa ofisini na watu wasiojulika,waliomshambulia kwa mapanga hadi kupoteza maisha,mnamo Oktoba 11.


Mratibu wa Mtandao huo,Onesmo Olengurumwa,amesema ni mauaji ya kinyama,yanayohitaji sauti nyingi za kulaani,ili mamlaka ziharakishe uchunguzi,na kubaini wahusika,ili Sheria ichukue mkondo wake,ili kuwaondolea hofu Watendaji wengine,ambao kwa namna yoyote,tukio hilo limewaathiri Katika majukumu yao.


"Watendaji watashindwa kutekeleza majukumu yao kwa hofu ya usalama,na hatimae kushindwa kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo ya Wananchi",amesema Olengurumwa Katika mahojiano maalumu na Watetezi Media.


Mtandao huo pia,umetoa Rai kwa taasisi zingine,kuungana,kukemea matukio ya namna hiyo,ambayo endapo yataachwa na kupita,madhara yake ni makubwa kwa viongozi wa ngazi mbalimbali,wanaoshughulika na Wananchi moja kwa moja kila uchwao.


"Mfano Watendaji,ndio viongozi wetu tunaokaa nao mtaani kila siku,na ndio wanasikiliza kero zetu",ameonge Olengurumwa.


Marehemu Kelvin,atazikwa kesho,Oktoba 14,Katika makaburi ya Ununio,yaliyoko Mbezi,na taratibu za kuaga mwili zitaanzia nyumbani kwa wazazi wake,eneo la Mbezi Makonde.


Watetezi Tv

October 13

Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI