.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth leo amefika Mbagala Majimatitu kutembelea katika kiwanja cha UWT Wilaya ya Temeke ambapo ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Umoja wa Wanawake Wilaya ya Temeke unaendelea akiongozana na Mwenyekiti wa UWT Temeke Ndugu Rukia Kamal, Viongozi wa Kata, Matawi na wajumbe wa Kamati ya ujenzi wa nyumba ya hiyo.
Mh. Mahawanga amefurahishwa na hatua nzuri inayofanywa na Kamati ya ujenzi pamoja na UWT Wilaya kwa kusimama vyema hatua za awali za ujenzi wa nyumba hiyo ambapo naye aliwaunga mkono na kuwakabidhi Tani tano 05 za saruji ili kutekeleza ahadi yake ya kuunga mkono ujenzi wa nyumba za Watumishi wa UWT Wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa tani tano kwa kila Wilaya ambapo jana alianza na Kinondoni na leo amekabidhi Temeke.
Aidha Mh. Mahawanga amesisitiza kuendelea kushirikiana nao kwenye kila hatua za ujenzi ili kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika kwa uharaka zaidi lakini pia kuhakikisha Jumuiya ya Wanawake inazidi kuwa imara.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Ndugu Rukia Kamal amempongeza Mh. Mahawanga kwa utekelezaji wa ahadi yake mapema na kumuhakikishia kamati itasimamia vyema ujenzi huo na watazidi kushirikiana pamoja na endapo patakuwa na changamoto watajuzana ili kuweza kufikia lengo la kukamilisha ujenzi. Pia amempongeza sana kwa kwa kazi nzuri anayofanya ya kuhakikisha anatoa Elimu kuhusiana na vikundi ili kuweza kufikia lengo kuu la kuwainua na kuwakwamua wanawake kiuchumi.





0 Comments