Header Ads Widget

ULIPAJI WA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI WA NDANI BADO NI KITENDAWILI.

Na chausiku Said MDTV Mwanza.

Ulipaji wa misharaha kwa wafanyakazi wa ndani bado ni Changamoto inayosababisha kutofikia malengo yao.

Afisa Usimamizi Makao na uwezeshaji kutoka shirika la Wote Sawa Demitila Faustine ameeleza kuwa changamoto hizo hulepekea wasichana hao wakazi kuingia kwenye migogoro na waajiri wao.

Demitila ameeleza kuwa waajiri kutowalipa kwa wakati mfanyakazi wao mishahara hupelekea kuingia kwenye  migongano.

Amesema kuwa waajiri kuwapa nafasi na kutambua umuhimu wa kuwasilikiza na kuongea na wao kutambua majukumu yao ili kuepukana na migogoro hiyo isiyo kuwa na ulazima.


Hata hivyo wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto shule na sio kuwapeleka kufanya kazi za ndani chini ya umri mdogo.

Glory Shindika mkaguzi wa polisi kutoka dawati la jinsia ameeleza kuwa dawati la jinsia linasikiliza malalamiko yote ya ukatili wa kijinsia na kuelimisha jamii kwa ujumla.

ameeleza kuwa jamii inayowajibu wa kumuona mfanyakazi  wa ndani ana umuhimu na kuweza kumsaidia kufikia malengo yao.

Afisa kazi Mwanza Bietty Mteja ameeleza kuwa sheria imemtambua mfanyakazi wa ndani na kuweza kufikia hatua ya kuweka kima cha mshahara na kuweka haki zao za msingi

Biety ameeleza kuwa Jamii bado inamtazamo mdogo kwa mfanyakazi wa ndani na kuona kazi hiyo sio kama kazi zingine ambazo watu wengine wanafanya, na kutofahamu wajibu wa wafanyakazi hao.

Kwa upande wake Neema Jackobo ambaye ni mfanyakazi wa ndani ameeleza kuwa wanawajibu wa kusimamia na kupaza sauti pale wanapopitia ukatili na changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili wa kimwili na kingono.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI